JAJI MGEYEKWA AWAITA WANANCHI KUJIFUNZA USULUHISHI MIGOGORO YA ARDHI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 24, 2023

JAJI MGEYEKWA AWAITA WANANCHI KUJIFUNZA USULUHISHI MIGOGORO YA ARDHI

 

Katika kuadhimisha wiki ya sheria, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imeandaa siku moja ya kutoa elimu na kukutana na wadaawa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu Dar es Salaam siku ya Alhamisi Januari, 26, 2023.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi Mhe. Agnes Mgeyekwa amesema siku hiyo Majaji wa Mahakama yake watakuwepo katika viwanja hivyo  kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujifunza faida za usuluhishi katika masuala mazima ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Kwa mujibu wa Mgeyekwa, Majaji wa Mahakama hiyo watakuwemo katika Banda hilo la Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi kuanzia saa 3 asubuhi hadi 9 alasiri ambapo watatoa elimu na kukutana na wadaawa.

"Ninawaomba wananchi wajitokeze kwa ajili ya kujifunza faida za usuluhishi katika utatuzi wa migogoro ya ardhi". Alisema Jaji Mgeyekwa.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad