Kambi maalum ya matibabu na upimaji wa moyo yafanyika Zanzibar - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 25, 2023

Kambi maalum ya matibabu na upimaji wa moyo yafanyika Zanzibar

 

 

Afisa Uuguzi wa Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Tumpale Kionjola akimpima shinikizo la damu mwilini (BP) mama Amina Marzuk aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar leo kwa ajili ya kupata huduma ya  upimaji na matibabu ya moyo. JKCI kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanyaka kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima.
Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimuuliza maswali mama Mwajuma Kidawa aliyefika leo katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji na matibabu ya moyo yanayofanyika katika hospitali hiyo. JKCI kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanyaka kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima.

Mfanyakazi wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar Yasir Ally akimpima urefu na uzito mtoto aliyefika katika hospitali hiyo leo kwa ajili ya kupata huduma ya  upimaji na matibabu ya moyo. Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima.

Afisa Uuguzi wa Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) John Mirisho akimpima kipimo cha kuangalia wingi wa sukari mwilini Othman Maulid aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar leo kwa ajili ya kupata huduma ya  upimaji na matibabu ya moyo. JKCI kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanyaka kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad