Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo katika kikao na Watendaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakiongozwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe.
Kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 13 Januari, 2023 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma kilikuwa cha kupokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ya utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Tano wa Bunge.
No comments:
Post a Comment