BODI YA BONDE YA WAMI /RUVU YAPANDA MITI MTO KIZINGA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 26, 2023

BODI YA BONDE YA WAMI /RUVU YAPANDA MITI MTO KIZINGA


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV 

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu  imepanda miti kando kando ya Mto Kizinga  eneo la Buza Manispaa ya Temeke ikiwa ni kulinda vyanzo vya maji pamoja wananchi wanaendelea huduma ya maji katika Mto huo.

Akizungumza wakati wa upandaji Miti Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya  ya Temeke Thabit Mohamed lililifanyika eneo la Mto Mzinga amesema kuwa miti hiyo wananchi waitunze kwani baadaye ina faida kwa wananchi na mto kuendelea na utiririshaji maji.

Mohamed amesema kuwa wanannchi wanaoishi kando kando ya mto huo kuacha mara moja utiririshaji wa maji kutoka kwenye nyumba zao kwenda kwenye mto Mzinga 

Nae Afisa wa Kidakio cha Pwani Halima Faraj amesema kuwa Rais Dk.Samia Hassan Suluhu anataka wananchi wapate huduma ya maji na kuelekeza fedha ya nyingi kwenye miradi ya maji hivyo kazi ya wananchi kulinda vyanzo vya maji.

Halima amesema kuwa upandaji wa miti hatua ya kutaka kulinda mazingira na kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ambayo madhara yake kwa wananchi wameshaona ni pamoja na mafuriko.

Amesema kuwa wakati umefika kwa wananchi kuacha kujichukulia maeneo ya kando kando ya mito na kuendesha shughuli za kilimo kwani kwa kufanya kilimo hatua zitachukuliwa bila kuangalia macho yao yakionyesha kuonewa huruma.

Aidha amesema kuwa jukumu la ulinzi wa vyanzo vya maji hauko mikononi mwa bonde wala watoa huduma wa maji Dawasa bali ni jukumu la watu wote kwa kila mmoja anahitaji maji.

Afisa Mazingira wa Manispaa ya Temeke Wasiwasi Kaguo amesema kuwa wananchi wa kando kando ya mto kuacha kujenga eneo la mito kwani wataofanya hivyo kazi yao haitakuwa na uzito watachofanya ni kubomoa.

Amesema Serikali imetumia gharama za kununua miti ya matunda na miti ya kulinda vyanzo vya maji ambapo matunda hayo watakula wenyewe huvyo miti hiyo inahitaji usimamizi wa hali ya juu.

Meneja wa Mtambo wa Mtoni   wa Dawasa Hilder Razalo amesema kuwa ulinzi wa vyanzo  ni jukumu la mmoja kwani mazingira yakiharibika hayagusi mtu mmoja bali ni wote na serikali kuingia gharama.Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Thabit Mohamed akizungumza na wananchi walioko kando kando ya Mto Mzinga mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti.Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Thabit Mohamed akipanda mti kando kando ya Mto Mzinga Buza.Afisa wa Kidakio cha Pwani Halima Faraji (Mwenye kilemba cha rangi ya Samawari 'Blue') akipanda mti kwenye kando kando ya mto Mzinga , Buza Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.Afisa wa Kidakio cha Pwani Halima Faraj akizungumza ma wananchi wa Buza wakati wa zoezi la upandaji miti kando kando ya mto Mzinga jiijini Dar es Salaam.Meneja wa Mtambo wa Mtoni  wa Dawasa Hilder Razalo akizungumza kuhusiana na utunzaji wa mazingira katika vyanzo vya maji wakati zoezi la upandaji mito katika Mto Mzinga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad