Waziri Simbachawene ahimiza wananchi kutunza mazingira Inb - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 15, 2022

Waziri Simbachawene ahimiza wananchi kutunza mazingira Inb

 

 

Na Mwandishi wetu

Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amehimiza wananchi kuendelea kulinda na kutunza mazingira na kuhifadhi maeneo ya vyanzo vya maji.

Kauli hiyo imetolewa  katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi kijiji cha Mkoleko  Jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

“Tuanzishe mradi wetu wa maji kupitia vyanzo vya maji tulivyonavyo kwenye Mlima, ili tupate maji ya uhakika  kwa ajili ya shughuli za kijamii.”

Aidha  watendaji wa kata muendelee kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi ,ikiwa ni sambamba na kutunga sheria ndogo ndogo ili kuzuia ukataji wa miti katika kingo za makorongo ili kuzuia mmonyoko.

“Kama una miti pembezoni mwa shamba lako iache usiikate ili iendele kuzuia mmonyoko wa ardhi, inayoharibu miundo mbinu ya barabara.”

Waziri Simbachawene ameahidi kuendelea kuimarisha barabara zinazounganisha vijiji vyote vinavyounganisha kata ya Mansa kwa kuhakikisha barabara hizo zinafanyiwa ukarabati katika maeneo korofi.

Akimkaribisha Waziri, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa Mhe. Richard Maponda amemshukuru Waziri Simbachawene kwa jitihada zake za kuleta maendeleo katika Halmashauri ya Mpwapa, kuna zahanati sita zimefunguliwa na watu wanapata dawa.

“Kuna shule zimepata usajili ambazo zitasaidia kutatua adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.”

Naye Bwn. Emmanuel Nzoka ameshukuru serikali kupitia kwa mbunge kwa kutengeneza barabara na kuwa katika hali nzuri katika majira yote ya mwaka.

“Tulikuwa kisiwani kutokana na barabara kuharibika kutokana na maji ya mvua hivyo kushindwa kupitika katika majira ya masika.”


Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi katika Mkutano wa aliofanya katika Kijiji cha Mkoleko.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipotembelea zahanati ya Winza.Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipotembelea boma la nyumba ya walimu  katika shule ya Msingi Makose


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad