RE: MHE. SENYAMULE AKABIDHI ZAWADI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 26, 2022

RE: MHE. SENYAMULE AKABIDHI ZAWADI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo tarehe 24 Desemba2022 amekabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu za Krismasi na mwaka mpyakatika kituo cha Safina kilichopo Ntyuka Jijini Dodoma kwa niaba ya Mhe. DktSamia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na Mchele, Unga wa Ngano, Sabuni, Sukari,
Mafuta, vinywaji pamoja na mbuzi wawili. Amesema zawadi hizo ni kwa ajili ya
kukidhi mahitaji ya watoto katika kipindi hiki cha sikukuu.

Amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ametuma salamu za Upendo na kuwaomba watoto hao kukua katika
maadili ya kumpendeza Mungu na wanadamu.

“Lengo na dhumuni la Mhe. Rais ni kuona watoto wanasheherekea sikukuu kwa
furaha na amani, kumbukeni kuwa chochote anachokifanya ni kwaajili ya
watanzania wote ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa ili watoto mpate elimu
bora na kuongeza kiwango cha utafulu, hivyo mkiwa darasani msikilize mwalimu
na mkirudi kituoni muda wa jioni jisomeeni” Alisisitiza Mhe. Senyamule.

“Chochote unachokifanya fanya kwa bidii kila mtoto ana ndoto na malengo yake
ya baadae, Serikali inatambua mchango wenu ndio maana Dkt. Samia Suluhu
Hassan ameamua kutoa zawadi hizi za vyakula na kiasi cha fedha ili wote
mfurahie sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya. Mhe. Senyamule aliongezea.

Mhe. Senyamule amewashukuru waangalizi wa watoto hao kwa kujitoa kwao
kuwalea katika maadili mema na kumuomba Mungu kuendelea kuwabariki
Walezi na wahudumu wengine katika malezi ya watoto hao.

“Jukumu lenu ni pamoja na kuhakikisha watoto hawa wasoma ili kuyatumia
madarasa yanayojengwa na Serikali chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan ili tuwe na kizazi chenye maadili mema ya kitanzania na ndoto za
kutimiza malengo ya watoto wetu” Alifafanua Mhe. Senyamule.

Aidha mlezi wa kituo cha Safina Bi. Neckson William ameishukuru Serikali kwa
kutoa zawadi za sikukuu kwa watoto.

“Tunaishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kutusaidia kituo cha Safina tumefurahi sana kwakuwa tuna
watoto ambao pia wapo nje ya Safina. Kituo kinawatoto kuanzia miaka miwili na
mwaka huu tumefanikwa kupeleka Chuo Kikuu watoto wawili” Alisisitiza Bi.
William

Kituo cha Safina kilianzishwa mwaka 2004 na kina jumla ya watoto 40, wavulana
35 na wasichana 5 pia kitua hicho kinawasaidia watoto ambao wanatoka katika
mazingira magumu. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad