ONANA ABWAGA MANYANGA CAMEROON - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 23, 2022

ONANA ABWAGA MANYANGA CAMEROON

 

 

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Golikipa wa Kimataifa wa Cameroon, Andre Onana rasmi ametangaza kustaafu kucheza timu hiyo ya taifa, ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo itoke kwenye Michuano ya Kombe la Dunia 2022 ambayo ilihitimishwa kwa Argentina kutwaa ubingwa huo.

Onana ametangaza kustaafu kucheza timu ya taifa ya Cameroon huku ikionekana kuwa Golikipa huyo amesusa kucheza timu hiyo ya taifa baada ya kutajwa kuwa kwenye mtafaruku baina yake na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Rigobert Song.

“Nitaendelea kuwa pamoja na Cameroon kwa Moyo wangu wote, Cameroon ni taifa langu, nitaendelea kupigania Bendera ya taifa langu kwa nguvu zote popote pale niendapo”, amesema Onana kwenye taarifa aliyoitoa ya kustaafu kucheza timu ya taifa.

Wakati wakiwa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, Onana alicheza mchezo mmoja pekee dhidi ya Switzerland katika michezo ya Kundi G la Michuano hiyo, huku akikosekana kwenye michezo miwili dhidi ya Serbia na Brazil.
Baada ya kukosekana kwenye mchezo wa pili dhidi ya Serbia, taarifa zilibaini kuwa Kocha wa timu hiyo ya Cameroon, Song alimuweka benchi Golikipa huyo kwa madai ya kuwa anatumia mbinu za zamani katika ulinzi wa lango, hivyo nafasi yake ilichukuliwa na Golikipa namba mbili wa timu hiyo, Devis Epassy.
Andre Onana alianza kucheza timu ya taifa ya Cameroon, Septemba 2016 alicheza michezo 34 pekee. Kwa sasa Golikipa huyo anacheza Klabu ya Inter Milan ya Italia akitokea Ajax ya Uholanzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad