Manyara Tanzanite Marathon Yafana, Washindi Wabeba Pesa na Medali - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 18, 2022

Manyara Tanzanite Marathon Yafana, Washindi Wabeba Pesa na Medali

 

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paluline Gekul  amezindua mbio za riadha za Manyara Tanzanite Marathon,  lengo ikiwa ni kutangaza utalii pamoja na kukuza na kuendeleza vipaji vya mchezo wa Riadha nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mbio hizo   Desemba 17,2022 Babati Manyara,  Mhe. Gekul ameeleza kuwa, Mkoa wa Manyara una vivutio vingi ikiwemo madini ya Tanzanite, Hifadhi ya Tarangire pamoja na Ziwa Babati ambapo  kupitia mbio hizo, vivutio hivyo vitatangazwa zaidi   na kuvutia  watalii ndani na nje ya nchi.

"Tunakusudia kuwa na Akademi ya riadha katika Mkoa wetu wa Babati, ambao asilimia karibu tisini ya wanariadha nchini wanatoka hapa, tunataka vijana wajiendeleze katika vipaji walivyonavyo vya kukimbia kwa kupitia marathon hii na hivyo kutoa fursa kwa vijana kuonesha uwezo wao na kupata kipato kwakua michezo ni ajira" amesema Mhe.Gekul

Ametumia nafasi hiyo kusisitiza Halmashauri, kutenga fedha kwa ajili ya michezo pamoja na kuhimiza wananchi kufanya mazoezi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kama maelekezo ya Serikali yanavyosema.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Neema Msitha amewasisitiza Waandaaji wa Marathon mbalimbali,  kuzingatia utaratibu wa kuandaa Mashindano hayo kwa kuwashirikisha Maafisa Michezo wa maeneo husika.

Bi. Msitha ametoa rai kwa Wazazi na Walezi kuruhusu watoto wao kushiriki michezo mbalimbali, huku akiwasihi wadau kujitokeza kuwekeza katika michezo ambayo imekua na fursa nyingi Duniani.

Naye Mshindi wa KM 42 upande wa Wanaume Elisha Wemma amesema Mashindano hayo yamempa uzoefu na kujiimarisha zaidi, ambapo amesema yamempa hamasa ya kushiriki mbio nyingi zaidi  za ndani ya nchi  na Kimataifa.

Marathon hiyo imeshirikisha mbio za KM 42, 21, 10 Mita 100, 400, na 1500 Kwa Wanaume na Wanawake, ambapo washindi wamepata zawadi ya pesa taslimu pamoja na Medali.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad