NAIBU WAZIRI KATAMBI AONGOZA KIKAO KAZI CHA TATHMINI NA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI MAJUKUMU OFISI YA WAZIRI MKUU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 23, 2022

NAIBU WAZIRI KATAMBI AONGOZA KIKAO KAZI CHA TATHMINI NA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI MAJUKUMU OFISI YA WAZIRI MKUU

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya ofisi hiyo hii leo tarehe 23 Disemba, 2022 katika jengo la OSHA, jijini Dodoma. Lengo la kikao kazi hicho ni kufanya tathmini na kupanga mikakati ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo.

Akizungumza na menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Katambi amewataka viongozi hao kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, ufanisi, kushirikiana na kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao ili kufikia matarajio ya Serikali na wananchi wanaowahudumia.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akisisitiza jambo kwa Menejimenti wakati wa kikao kazi cha kupitia na kutathmini utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Said Mabie akieleza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika tarehe 23 Disemba, 2022 katika jengo la OSHA, jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa menejimenti wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha kupitia na kutathmini utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo uliofanyika tarehe 23 Disemba, 2022 katika jengo la OSHA, jijini Dodoma.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya ofisi hiyo mara baada ya kuhitimisha kikao kazi cha kupitia na kutathmini utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo uliofanyika tarehe 23 Disemba, 2022 katika jengo la OSHA, jijini Dodoma. Wan ne kutoka kulia ni Kamishna wa Kazi, Bi. Suzan Mkangwa
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad