MAKUMBUSHO YA TAIFA YAKARIBISHA WANANCHI USIKU WA KAHAWA. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 23, 2022

MAKUMBUSHO YA TAIFA YAKARIBISHA WANANCHI USIKU WA KAHAWA.

 

Na Karama Kenyunko Michuzi TV 

MAKUMBUSHO ya Taifa ya Tanzania   imefungua milango kwa ajili ya kuwasaidia wasanii mbalimbali wa asili walio tayari kufanya kazi zao za sanaa ndani na nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa leo Desemba 22, 2022 jijini Dar es Salam na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Emmanuel Lugomela alipokuwa akiwakaribisha wakazi wa Dar es Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Kahawa la mwaka 2022 'Kahawa Night' litakalofanyika Desemba 30, mwaka huu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. 

 “Tumefungua milango kwa wasanii wa Tanzania ambao wana nia ya kutangaza kazi zao pamoja na kuwasaidia wasanii katika kufanya maonyesho ya kazi zao ndani na nje ya nchi,” amesema. Lugomela.

Amesema kuwa Tamasha la Usiku wa Kahawa  litaenda sambamba na uzinduzi wa Orodha ya Nyimbo za nyongeza (EP) kutoka kwa msanii kutoka Tanzania Regina Kihwele maarufu Gynah ambaye ni mwimbaji mahiri wa kimataifa, mtunzi wa nyimbo, mwigizaji, mwanamitindo na mwanaharakati wa afya ya akili. 

Pia ameongeza kuwa katika kazi zake za sanaa Gynah amefanikiwa kushiriki matamasha mbalimbali ya kimataifa ambayo yamempa nafasi ya kujitangaza yeye na kuitangaza Tanzania kimataifa.

 Lugomela amesema mbali na uimbaji na uanamitindo msanii huyo alifanikiwa kushinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike barani Afrika katika tamasha la Filamu la 'Lake International Pan African' lililofanyika mwaka jana jijini Nairobi, Kenya.

 Amesema Regina aliteuliwa kuwa mmoja wa waigizaji wenye umri mdogo zaidi na Bodi ya Filamu Tanzania kwa nafasi yake ya mwigizaji msaidizi katika mfululizo wa filamu za "Mulasi the Death". 

 Lugomela amesema makumbusho ya Taifa yamekuwa yakiendesha programu ya kukuza  vipaji vya wasanii wa Jukwaani na wasanii wa Kazi za Mikono kwa miaka sita kwa kuwapa mazoezi kila siku ya Ijumaa ya mwisho wa mwezi. 

Kwa upande wake msanii Regina Kihwele amesema amejipanga vyema kutoa burudani katika Usiku wa Kahawa akisema vyakula mbalimbali vya asili vitaliwa sambamba na unywaji wa kahawa.

Akaongeza kiingilio katika tamasha hilo itakuwa Shilingi 5000/- kwa wanafunzi wakati tiketi maalum itagharimu 50,000/- kwa mtu na tiketi ya kawaida itakuwa 20,000/.

 “Tunawaomba watanzania waje kufurahia nasi Ijumaa wiki ijayo kwa sababu hii itatusaidia sana kukuza utamaduni wetu" amesema Regina. 

Tamasha la Kahawa Night limeandaliwa na Makumbusho ya Taifa kupitia kituo chake cha makumbusho na Makumbusho Art Explosion Program kwa kushirikiana na Tabasamy PR Consult. Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni,  Emmanuel Lugomela (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwakaribisha wakazi wa jijini Dar Es Salaam kwenye tamasha la lijulikanalo kama usiku wa Kahawa litakalofanyika ukumbi wa makumbusho ya Taifa Desemba 30,2022. Kushoto kwake ni msanii Regina Kihwele maarufu kama Ghyna  na kulia ni Chance Ezekiel Mkuu wa Idara ya Programu Makumbusho na Nyumba ya UtamadunMsanii Regina Kihwele Kushoto akizungumza wakati wa mkutano kuelekea tamasha lake  la Usiku wa Kahawa linalotarajiwa kufanyika Desemba 30,2022 jijini Dar es Salaam. katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni,  Emmanuel Lugomela na kulia Chance Ezekiel,  Mkuu wa Idara ya Programu Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.Mkuu wa Idara ya Programu Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Chance Ezekiel, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani,  kuelekea Tamasha la Usiku wa Kahawa likalotumbuizwa na Msanii Regina Kihwele maarufu kama Gynah. Wa katikati ni kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni,  Emmanuel Lugomela na kushoto ni  msanii Regina Kihwele.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad