MPOTO NA KUNDI LAKE WAALIKWA KATIKA TAMASHA KUBWA LITAKALOFANYIKA INDIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 13, 2022

MPOTO NA KUNDI LAKE WAALIKWA KATIKA TAMASHA KUBWA LITAKALOFANYIKA INDIA

 

 

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


MSANII maarufu nchini Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba na kundi lake la Mpoto Theatre wamealikwa nchini India kwa ajili ya kwenda kutoa burudani kwenye Tamasha la 
Pramukh Swami Maharaj Shatabdi Mahotsav.

Tamasha hilo limeaandaliwa maalimu kwa ajili ya kumbukumbu ya kifurahia maisha ya muasisi na Rais wa zamani wa  taasisi Bochaasaniwasi Aksharpurushottam Wsaminarayan ambayo imejikita kwenye masuala ya kibinadamu na kiutamaduni ndugu Makao makuu ya taasisi hiyo yako nchini India na inawachama walio hai duniani kote .Rais huyo anafahamika kwa jina la Pramukh Swami Muharaj.

Akizungumza leo Desemba 12,2022  akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar wa es Salaam akielekea nchini India , Mpoto amesema anakwenda kwenye Tamasha hilo kwa mualiko maalimu kutoka kwenye taasisi hiyo

Ameongeza kuwa tamasha hilo litafanyika kwenye viwanja venye ukubwa wa Hekta 100 katika eneo la Ahmedabad ,Gujarat ,India na watakaohudhuria watafurahia mambo ya kimilia na kiimani yanayovutia.

"Kwanza tunawashukuru waandishi wa habari kwa mchango wao mkubwa na msaada kwa wasaniii.Leo tuko hapa kwa ajili ya kuwaaga  Mpoto Theater tumepata baraka na bahati kubwa ya kushiriki kwenye tamasha kubwa kabisa duniani linalofanyia pale nchini ambalo litachukua siku zisizopungua 38 mpaka 40.

"Tamasha hili linaitwa Pramukh Swami Muharaj kwa ajili ya kusherehekea muasisi wao wa taasisi hii na Rais wa zamani ambaye anatimiza miaka 100. Kwa hiyo Wahindi wote  wa madhehebu hayo na watu kutoka Dunia nzima wanakutana pale ambapo wanasherehekea kuanzia katikati ya Desemba hadi katikati ya Januari lakini wanakutana kwenye eneo kubwa.

"Watu milioni 15 wamethibitisha kushiriki hadi sasa na walioweka nafasi ( Booking) kwenda kuangalia  kutoka Tanzania na Afrika ni watu 56,000 kwa siku, kwa hiyo watu wanaendelea kufanya booking kuja kuangalia onesho letu la Mpoto Theatre,inaonekana watu wanatusubiria kwa hamu kubwa,"amesema Mpoto.

Aidha Mpoto amesema wanatoa shukrani za kipekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwani bila yeye kufungua fursa na milango hiyo  nadhani mataifa mengi wasingewaona." Sasa wasanii wanapata mialiko mingi nje ya nchi ,ni kwasababu filamu yake ya Royal Tour imesaidia watu wengi waonekane kutokea mbali , wakasema Afrika Tanzania kuna Mpoto.

"Watu  ambao wamejipambanua kwenye sanaa za kiafrila kwa hiyo tunashukuru, tunasema Mheshimiwa Rais ahsante sana na Serikali ya Awamu ya Sita lakini kikubwa sisi tunaahidi dhamana tuliyopewa, Imani tuliyopewa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutakuwa wawakilishi wema."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad