WANANCHI WA WILAYA YA SONGWE WAMEJAWA NA MIOYO YA SHUKRANI KWA RAIS MHE. DR. SAMIA SULUHU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 29, 2022

WANANCHI WA WILAYA YA SONGWE WAMEJAWA NA MIOYO YA SHUKRANI KWA RAIS MHE. DR. SAMIA SULUHU

 

Mkuu wa Wilaya ya Songwe,Simon Simalenga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Wakulima wa Wilaya ya Songwe, Mkoa wa Songwe wanaufaika na upatikanaji wa Mbolea ya Ruzuku ambapo mpaka sasa tayari kata za Gua,Kapalala, Ngwala, Saza na Mkwajuni  Wilayani Songwe zimenufaika na mgao huo kwa kupokea jumla ya mifuko 10,912 huku mbolea zaidi ikitarajiwa kupokelewa hivi karibuni.

Simalenga ametoa shukrani hizo kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Songwe alipofanya ziara maalum ya kukagua maghala ya Mbolea kwenye Kata hizo za Tarafa za Songwe na Kwimba hivi karibuni.

“Hakika wananchi wa Wilaya ya Songwe wamejawa na mioyo ya shukrani kupita kiasi kwa Rais wetu mpendwa Mhe. Dr. Samia SULUHU Hassan bila kumsahau Waziri wetu wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (MB) kutokana jitihada kubwa zinazoendelea kufanyika kwa Wakulima wa nchi hii na sisi Songwe tukiwemo kwasababu mpaka sasa tunaendelea kupokea Mbolea kila wiki na muitikio wa Wananchi ni mkubwa sana, hizi changamoto ndogo ndogo nilizopokea ikiwemo ucheleweshwaji wa mbolea kwa baadhi ya maeneo tayari nimeshawasilisha kwa Mkuu wetu wa Mkoa MHE. Waziri Kindamba ambaye mara zote amekuwa msaada mkubwa katika kushughulikia masuala ya Songwe kila tunapomshirikisha.” Alisema SIMALENGA

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad