DC MGEMA AWAPONGEZA MANISPAA YA SONGEA KUKAMILISHA UJENZI WA MADARASA 76 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 20, 2022

DC MGEMA AWAPONGEZA MANISPAA YA SONGEA KUKAMILISHA UJENZI WA MADARASA 76

 

 


NA STEPHANO MANGO, SONGEA

MKUU wa Wilaya ya Songea Pololet  Mgema  ametoa pongezi kwa Wataalamu na Viongozi wa Manispaa ya Songea  katika kufanikisha kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa 76 ambavyo vimekamilika.

Mgema alisema lengo kuu la kutembelea miradi hiyo ni kufanya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa 76, viti na madawati ili  kujiridhisha na  hatua iliyofikia kwa kila mradi kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023.

Alisema Wilaya ya Songea ilipokea  fedha za kujenga madarasa 96, kati ya hayo madarasa 10 yamejengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, madarasa 10 katika Halmashauri ya Madaba na madarasa 76 yamejengwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambayo ujenzi wake umekamilika. “ Mgema alipongeza”

Hayo yamejili katika ziara ya ukaguzi wa miradi iliyofanyika jana ambayo iliongozwa na kiongozi huyo ambapo alitembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa 3 katika shule ya Sekondari Sili, ujenzi wa vyumba vya madarasa  6  katika shule ya Sekondari Luwawasi, ujenzi wa vyumba vya madarasa 6  shule ya Sekondari Lizaboni, madarasa 6 shule ya Sekondari Chandarua, madarasa 2 sule Sekondari Matogoro, madarasa 3 shule ya Sekondari   Mashujaa pamoja na ujenzi wa madarasa 2 shule ya Sekondari Mateka.

Aliongeza kuwa Mafanikio yaliyopatikana yametokana na ushirikiano kati ya wataalamu na viongozi mbalimbali ambayo yamesaidia kuonesha taswira nzuri  ya  usimamizi imara wa miradi Mkoani Ruvuma.

Mgema ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha shilingi  Bil.3.2  kwa ajili ya kujenga madarasa 156 Mkoa wa Ruvuma kati ya hizo Manispaa ya Songea ilipokea kiasi cha fedha Bil. 1.52 ambazo zimetumika kujenga madarasa 76 ambayo ujenzi wake umekamilika. “Alishukuru.”

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko alisema kuwa Manispaa ya Songea inatoa shukrani kwa Serikali ya wamu ya sita kwa kutoa fedha Bil. 1.52 kwa ajili ya  ujenzi wa vyumba vya madarasa 76 ambayo  yamejengwa na kukamika na tayari kwa kuyakabidhi kwenye  ngazi za juu za kiutawala

Dkt Sagamiko ametoa rai kwa wataalamu na Waheshimiwa Madiwani kuongeza jitihada katika kusimamia ujenzi wa majengo mengine kwenye miradi ya sekta ya afya , miundombinu na ukusanyaji wa mapato ya ndani

Alisema kuwa pongezi ya kazi ambazo tunazipata iwe chachu ya kuendelea kujituma kwa ueledi mkubwa ili kufikia malengo kusudiwa katika mipango mbalimbali ambayo tumejiwekea katika Manispaa yetu

Naye Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Maiko Mbano alisema Halmashauri ya Manispaa ya Songea katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi October imepokea jumla ya Tshs 2,757,250,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Elimu, Afya, Maendeleo ya Jamii na Utawala.

Mbano alisema kuwa watumishi wa Manispaa hiyo wamejipanga kikamilifu kutekeleza miradi yote kama ilivyopangwa ili iweze kuleta tija kwa wananchi

Amewataka wataalamu hao kushirikisha wananchi kila wanapotekeleza mradi kwenye kata husika ili kuleta uwazi na ushirikishwaji jamii ambao utaleta ulinzi shirikishi katika kulinda  rasilimali za umma ikiwemo kuundwa kwa kamati za ujenzi  ambazo zinajumuisha wanajamii. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad