CHOKOCHOKO ZA KISIASA NI HATARI KWA UMOJA WA KITAIFA - SHAKA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 17, 2022

CHOKOCHOKO ZA KISIASA NI HATARI KWA UMOJA WA KITAIFA - SHAKA

 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM melaani kauli za baadhi ya wafuasi, wanachama na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzi Zanzibar zenye kuhubiri mgawanyiko na kuchochea uvunjifu wa amani.

Shaka ameyasema hayo leo Desemba 17, 2022, wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyi yaliyofanyika kisiwani Pemba.

"Chama Cha Mapinduzi kinalaani vikali vitendo vilivyoanza kujitokeza siku za karibuni hasa kisiwani Pemba kwa baadhi ya wafuasi, wanachama na viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa kuhubiri mgawanyiko kuchochea uvunjifu wa amani, sio utamaduni wetu wazanzibari, sio utamaduni wetu Watanzania, CCM inalaani vikali, alisema.

Ameema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 Ibara ya 9(a) imeahidi katika kipindi cha miaka mitano kazi kubwa itakayofanywa na CCM ni kuimarisha maridhiano, kulinda amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Shaka amesema kazi hiyo inafanywa vizuri na Rais Dk. Samia na Rais Dk. Mwinyi. "Kuweni na amani wana CCM. Hamtajutia kumwani Dk. Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, nia yake ni kutuvusha."

Katibu Mwenezi Shaka amesema Rais Dk. Samia na Rais Dk. Mwinyi ni nyenzo muhimu katika kuendeleza mapatano, maridhiano na masikilizano ya kisiasa nchini. 

"Wameanza vizuri sana kwa sababu wana baraka za Chama Cha Mapinduzi," alisema.


MAMLAKA YA RAIS YAHESHIMIWE

Shaka amesema uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar haujamwondolea Rais Dk. Mwinyi mamlaka ya kikatiba kufanya shughuli za kiutawala.

Amesema Dk. Mwinyi hapangiwi, bali anashauriwa na kwenye kushauriwa kuna kukubali au kukataa, hivyo jpokuwa kuna serikali ya umoja wa kitaifa, lakini Katiba ya nchi lazima iheshiniwe.

"Uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa sio sababu ya kujihalalishia kwamba eti kuna chama kingine ni lazima kishinde uchaguzi hapana. Wenye ulazima wa kushinda uchaguzi ni CCM ambao tumebeba dhamana ya kuwatumikia Wazanzibari tumebeba dhamana ya kuwatumikia Watanzania kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, kazi hiyo imefanywa vizuri sana na Dk. Mwinyi," amesema.

Aidha, alimhakikishia Dk. Mwinyi kuwa Wazanzibari Watanzania kwa ujumla hususan wapenda maendeleo wanamwlewa, hivyo aendelee kuchapa kazi.

"Uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa sio Jukwaa la fursa na kutaka kuleta mgawanyiko, mfarakano na kuvuruga amani ya nchi hatujafikia huko," alisema.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM Zanzibar) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akivikwa skafu baada kuwasilikatika Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa mapokezi rasmi visiwani humo baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM Zanzibar) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Pemba baada kwa ajili ya mapokezi rasmi visiwani humo baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti. (Picha zote na Fahad Siraj wa CCM).


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM Zanzibar) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika gari la wazi akisalimia wananchi waliokusanyila barabarani kumlaki baada kuwasili Mkoa wa Kusini Pemba kwa ajili ya mapokezi rasmi visiwani humo baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM. 
Mke wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM Zanzibar), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, Mama Mariam Mwinyi akipiga kufi kushangilia jambo wakatika wa mapokezi ya Dk. Mwinyi kisiwani Pemba baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM. 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM Zanzibar) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wana CCM wakati hafla ya mapokezi yake rasmi kisiwani Pemba baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM. 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa hafla ya mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM Zanzibar) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, iliyofanyika Mkoa wa Kusini Pemba.

Baadhi ya Wana CCM wakiwa katika shamrashamra za mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM Zanzibar) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi yaliyofanyika kisiwani Pemba.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad