WANANCHI WA MKOA WA LINDI KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA KIBINGWA. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 3, 2022

WANANCHI WA MKOA WA LINDI KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA KIBINGWA.

 

NA WAF- DOM

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema, wananchi wa Mkoa wa Lindi wanatarajia kuendelea kunufaika na huduma za kibingwa, baada ya Serikali kuendelea kusomesha Madaktari bingwa ambao wataenda kutoa huduma hizo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.

Dkt. Mollel amesema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu Mhe. Tecla Mohamedi Ungele  katika kikao cha tatu cha bunge la 9 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jijini Dodoma. 

Amesema, katika kuongeza idadi ya madaktari bingwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, Wizara imepeleka kusoma jumla ya madaktari 7, ambao wataenda kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi

Akifafanua zaidi, Dkt. Mollel amesema, katika madaktari bingwa 7 wataoenda kupata mafunzo, madaktari 2 wanasomea udaktari bingwa wa watoto, Ubingwa wa upasuaji 2, Daktari bingwa wa Mionzi 1, Daktari bingwa wa Mifupa 1 na Daktari bingwa wa Afya ya Uzazi na watoto 1.

Aidha, Dkt. Mollel amesema, Serikali inakamilisha taratibu za uhamisho ili kupata daktari bingwa wa magonjwa ya ndani ili wananchi wa Mkoa wa Lindi waweze kunufaika na fani hiyo.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad