Wanakijiji wa kijiji cha Malolo, Kata ya Malolo wilayani Ruangwa mkoani Lindi, wameanza kutekelezaji mkakati wa kupanda miti 16000 katika eneo la hekali 50 kwa lengo la kuendelea kutunza mazingira kijijini hapo.
Hayo yameelezwa mapema leo na kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Abdalah Lyuba, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kwa lengo la kujionea matokea ya mradi wa kuhifadhi misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya mazao ya misitu Tanzania (CoForEST), unaotekelezwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) kwa kushirikiana na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo na
Ushirikiano la Uswisi (SDC).
Lyuba alisema kuwa kijiji cha Malolo ni miongoni mwa vijiji 41 nchini vinavyotekeleza mradi wa CoForEST ambapo jumla ya hekali 1589 za msitu wa asili wa kijiji hicho umehifadhiwa kwa mbinu za
uhifadhi shirikishi na uvunaji endelevu wa mazao ya misitu.
“Kipee tunashukuru ujio wa mradi huu wa CoForEST ulioanza kutekezwa kijijini hapa mwaka
2021, ambao umetupa hamasa kubwa ya kuhifadhi mazingira na misitu yetU, hivyo kwa pamoja
tuliazimia kuanza kupanda miti 16000 katika eneo la hekali 50 kwa lengo la kurejesha uoto uliopotea.”
Alisema Lyuba.
Lyuba aliongeza kusema kuwa tayari mpaka sasa wamekwisha panda miti 640 katika eneo la hekali
mbili huku wakiwa wamejiwekea malengo kupanda miti 16000 katika eneo la hekali 50.
Akitoa taarifa ya hali ya uhifadhi wa msitu wa asili wa kijiji hicho, Lyuba alisema kuwa msitu huo kwa
sasa unalindwa na kamati ya maliasili ya kijiji hali
iliyoufanya kuwa salama bila kuharibiwa na wavamizi.
“ Elimu ya Uhifadhi imebadili fikra za wananchi wote wa kijiji hiki, kwa sasa kila mwananchi ni mlinzi
wa msitu wa hifadhi wa kijiji na hakuna uvamizi wa uvunaji wa mazao ya misitu holela wala shughuli za
kibiadamu zinazohatarisha uhai wa msitu.” Alisema Lyuba.
Naye Modesta Hokororo Katibu wa kamati ya maliasili kijiji hapo alisema kuwa TFCG na MJUMITA
wamewapatia mafunzo mujarabu ya kulinda rasilimali za misitu hivyo kamati yake imejipanga
kikamilifu kuhakikisha msitu wa asili wa kijiji hicho unaendelea kuhifadhiwa na mazao yake kuvunwa kwa njia endelevu pasipo kuharibu bioanuai ya msitu huo....jpg)
...jpg)
No comments:
Post a Comment