Wadau wa Elimu waendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wanachangia kwa vitendo kuboresha mkakati wa kuhakikisha wanafunzi nchini wanasoma na kupenda masomo ya sayansi.
Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Abdul Maulid amepongeza Kampuni ya Baobab Shalom kuzindua Jarida la Sayansi lit litakalo muaanda mtoto na mzazi nje ya maisha ya shule aweze kuongeza ujuzi katika kukusanya taarifa, na kutafiti majibu sahihi ambapo itawezesha kufanya maamuzi binafsi pevu na yenye uhuru.
Akizungumza katika uzinduzi wa Jarida la Kisayansi liitwalo - OYLA Africa jijini Dar es Salaam Jana, Maulid amesema Serikali imewekeza said ya shilingi biliioni 100 kwa.ajikinwa ujenzi wa Shule za Sayansi nchini.
"Napongeza uwepo wa Jarida hili la OYLA Africa nchini, litasaidia kuwapa maarifa wanafunzi wetu kupata taarifa za kisayansi na litatumika katika shule zetu ikiwemo inavyotakiwa kujengwa eneo la Ubungo mkoani hapa, watoto watisoma na walimu watalitumia kufundishia," amesisitiza.
Meneja wa OYLA Africa Godfrey Lugalambi amesema jarida litawawezesha watoto kupata taarifa sahihi za kisayansi na kujua namna ya kuzuia magonjwa yanayoambukiza duniani. Pia kuwawezesha watoto kuwa na uwezo wa kuchunguza, kukusanya taarifa na kuzikabili changamoto za dunia iliyopo nje ya shule.
"Hii ni jarida bora kabisa na la kwanza la kisayansi kwa Tanzania na Africa yote. Ni chapisho la kila mwezi maalum kwa wanafunzi na wazazi ambapo limesheheni uchambuzi wa kisayansi, hisabati, fizikia na Tehama," ameeleza.
Amesema Jarida limechapishwa njia ya karatasi, ili kumrahisishia msomaji asilazimike kutumia intaneti au vifaa vya aina nyingine kupata taarifa japo huu ni ulimwengu wa digitali.
Mkurugenzi OYLA Africa Yevgemiy Semikov ametoa wito kwa wadau kuunga mkono jitihada hizo ikiwemo kupata nakala jarida hilo na kuendelea kushirikiana pamoja katika kuhakikisha linaboreshwa kwa ajili ya kuandaa kizazi kilicho bora kinachoweza kupambana na mazingira yanayowazunguka," ameeleza.
" jarida hili linaweza kusomwa na familia nzima, kuazimwa na marafiki na kutolewa kama zawadi kwa maktaba za shule. Jitihada zetu zinalenga kumwongezea mtoto maarifa na pia kuhakikisha inafikia walengwa wote sio shule tu za mjini lakini hata za vijijini," amesema Semikov.
Nae Mwakilishi kutoka Shule ya Sekondari Tusiime Jenipher Kaizilege amesema Jarida hilo la kisayansi limeandaliwa vema, limerahisisha vitu vingi na kuweka katika njia ya picha na michoro ambapo itamvutia mwanafunzi kusoma na kuelewa kwa haraka, nadharia imepeleka kwenye vitendo.
"Mwanafunzi ataitumia muda wake mwingi kulisoma badala ya kupekua simu janja ambapo analazimika kuona na mambo mengine yasiyofaa, pia litakuwa ni dhana ya kufundishia kwetu sisi walimu wa Sayansi kwa kuwa limesheheni vitu vingi sana," ameongeza Kaizilege.Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Abdul Maulid (katikati) akishirikiana naMkurugenzi OYLA Africa Yevgemiy Semikov kuzindua arida la Kisayansi liitwalo - OYLA Africa leo jijini Dar es Salaam (kulia) Meneja wa OYLA Africa Godfrey Lugalambi
(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)
No comments:
Post a Comment