SHAKA: RAIS SAMIA AMETENGA MABILIONI YA FEDHA KUIFUNGUA NCHI KWA BARABARA LAMI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 17, 2022

SHAKA: RAIS SAMIA AMETENGA MABILIONI YA FEDHA KUIFUNGUA NCHI KWA BARABARA LAMI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, amedhamiria kujifungia zaidi kwa mtandao wa barabara za lami na kuwaletea maendeleo wananchi.

Amesema Rais Samia amechukua hatua mbalimbali kuleta maendeleo ya wananchi wakiwemo wa Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Tabora.

Shaka ameyasema hayo leo Agosti 17, 2022, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Ushokola, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, wakati akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 katika ujenzi wa baraba katika Halmashauri hiyo.

“Nataka kuchukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo Watanzania, amenituma nije nikague barabara hii ambayo inajengwa kwa kilomita 2.7 hapa Kaliua, lakini kwenye wilaya hii Rais Samia ndani ya kipindi kifupi sana cha uongozi wake anakwenda kujenga barabara kilometa 10.

“Jambo ambalo halijawahi kutokea tangu nchi imepata uhuru na kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya Wilaya hii Rais Samia ndio anajenga barabara za lami. Anawajengea barabara lakini wakati huo huo anawawekea na taa inamaana Kaliua inakwenda kuwa ya  kileo.

“Kwa hiyo wote kwa pamoja tumpongeze Rais Samia, wote tumekuwa mashuhuda namna ambavyo Rais Samia amesimama kidete kufungua uchumi wa mtu mmoja mmoja, lakini uchumi wa kikanda na uchumi wa kimaeneo.

"Kukamilika kwa barabara hizi kilomita 10 ni hatua mpya ya kufungua uchumi wa wana Kaliua.Mtasafirisha mazao lakini mtarahisisha maisha yenu ya kila siku kwa kuhakikisha kuwa  huduma za kijamii zinapatikana kwa urahisi zaidi,” amesema Shaka.

Amesema Watanzania wanapaswa  kumshukuru Mungu kwa kuwa na Rais anayejua wananchi wake wanataka nini.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akisoma baadhi ya Nyaraka zilizowasilishwa kwake na mmoja wa Wananchi  kwenye mkutano wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akimvisha kanga ya Nyamitwe Maganga mkazi wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

Shaka akisikiliza kero kutoka kwa Nyandwi Dubo (aliyeshika vipazasauti) huku wananchi wakifuatilia mkutano katika Kijiji cha Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.

Shaka akicheza Ngoma yenye asili ya Wanyamwezi katika Kijiji cha Ushokola, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad