MWENYEKITI CCM UYUI ATOA YA MOYONI ZIARA ZA SHAKA, AMWAGIA SIFA LUKUKI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 21, 2022

MWENYEKITI CCM UYUI ATOA YA MOYONI ZIARA ZA SHAKA, AMWAGIA SIFA LUKUKI


Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Uyui

WEWE ni kiongozi wa kuigwa na tunakupongeza! Ndivyo anavyoelezea Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Lubasha Makoba, baada Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka kufanya ziara katika Kijiji cha Ufuluma wilayani Uyui mkoani Tabora .

Shaka ambaye anaandika historia ya kuwa  kiongozi wa kwanza wa CCM Taifa kufika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi , Wana CCM pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi .

Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi, Mwenyekiti wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Uyui Makoba, amesema Shaka anakuwa kiongozi wa kwanza kufika Kijiji Cha Ufuluma kwa ajili ya kufika kusikiliza changamoto zao pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

"Mgeni rasmi (Shaka) kwanza tukupongeze wewe binafsi na kwa niaba ya wana CCM kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Tanzania nzima, unastahili pongezi, sisi wana CCM tunakuona jinsi unavyofanya kazi, pia Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan) anakuona unavyofanya kazi vizuri.

"Anakuona  unavyowatumikia wana CCM Tanzania. Hongera sana Shaka.Ndugu kiongozi wetu, sisi tuna furaha kubwa ya wewe kutembelea Wilaya ya Uyui na ziara yako ina tija kubwa na hususan ulipotuelekeza wasaidizi wako unataka kwenda ukaonane na wananchi moja kwa moja, ni jambo la uzalendo wa hali ya juu,"amesema Mwenyekiti huyo.

Ameongoza kwamba kazi anazofanya Shaka katika kulitumikia Taifa la Tanzania amekuwa ni kiongozi wa mfano wa kuigwa, kwa sababu amekuwa akionekana maeneo mbalimbali ya nchi akisikiliza na kutatua kero za Watanzania na ziara zake zimekuwa na mafanikio makubwa.

"Umekuwa kiongozi wa mfano kwani umekuwa ukienda kusikiliza kero za wananchi na mafanikio yamekuwa makubwa, kwa hiyo nakupongeza sana," amesema Mwenyekiti huyo.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad