HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 12, 2022

MTANDAO WA ELIMU WAIZUNGUMZIA BAJETI MPYA YA ELIMU 2022/23



Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Ms. Faraja Nyalandu.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknlojia, Profesa Adolf Mkenda.

MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umeguswa na Bajeti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknlojia ya Mwaka 2022/23 iliyowasilishwa juzi bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknlojia, Profesa Adolf Mkenda.

Akiizungumzia Bajeti hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Ms. Faraja Nyalandu alisema kimsingi mtandao umeipokea kwa matumaini na kumpongeza Waziri, Prof. Mkenda kwa wasilisho hilo zuri, lililozingatia maoni ya wadau wa elimu.

"...Kimsingi tunampongeza sana Mh. Waziri wa Elimu Sayansi na Teknlojia, Profesa Adolf Mkenda kwa wasilisho zuri, kwani ni bajeti ambayo imegusa maeneo mengi, ambayo ni kipengele kizuri kwa maendeleo ya sekta ya elimu hapa Tanzania.

Alisema mchakato mzima wa bajeti hiyo umehusisha maoni ya wadau wengi wa elimu ikiwemo TEN/MET hivyo wanaamini hata wabunge wataipokea vizuri na kutoa maoni yatakayozidi kuijenga na kuleta mabadiliko katika sekta nzima ya elimu nchini Tanzania.

Akizungumzia maboresho kwenye sekta ya elimu kwa kuzingatia vipaumbele vya bajeti mpya, amesema bajeti inamwelekeo wa kufanya maboresho jambo ambalo linatia matumaini kwa wadau wa elimu hivyo kuishauri Serikali kuendelea kuwekeza zaidi na vizuri kwenye sekta ya elimu.

"..Tungependa kuona uwekezaji mkubwa zaidi kwenye sekta ya elimu hasa upande wa walimu, lakini hata kilichopo kwa sasa kitakuwa ni mwanzo mzuri na mwendelezo wa pale tulipoishia, tunafurahi pia kuona suala la elimu jumuishi limetiliwa mkazo, uwekezaji kwenye miundombinu  umetiliwa mkazo na hata uwekezaji kwenye taaluma nzima ya ualimu," alisema Ms. Nyalandu ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shule Direct.

ili kuwezesha utekelezaji wa malengo kwa bajeti hiyo mpya ya mwaka wa fedha 2022/23, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika bajeti yake imeliomba Bunge kuidhinisha jumla ya shilingi 1,493,004,355,000.00.

1 comment:

Post Bottom Ad