NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
WAUMINI wa Dini ya Kiislamu Jiji la Mwanza wameaswa kulinda amani,
utulivu na usalama wa nchi pamoja na wageni wakati wote wa sherehe za
Maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W, kwani amani ikivunjika wote
watahusika.
Rai hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Masheikhe wa Mikoa ya Kanda
ya Ziwa, Haruna Kichwabuta, kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa BAKWATA kwa
niaba na masheikhe hao wakati wa kupokea taarifa ya maandalizi ya
maulidi uliofanyika,kwenye Ukumbi wa Sheikhe Salum Ferej.
Sheikhe huyo wa Mkoa wa Kagera, alisema suala la amani na utulivu ni
muhimu, lakini ikivunjika waislamu wote watahusika,hivyo lazima
wajichunguze na kuwachunguza wengine wenye nia ovu wanaoweza
kujipenyeza ili kuvuruga amani, utulivu ili kuharibu jina la Uislamu
na Maulidi yenyewe.
“Waislamu tuhakikishe tunakuwa macho na watu wenye nia ovu wanaoweza
kujipenyeza miongoni mwetu wakati wa Maulidi ili kuchafua
Uislamu.Tunahitaji watu watakaokuja hapa watusaidie kulinda amani na
utulivu wa nchi yetu na kuhakikisha usalama unakuwepo.Pia tutakuwa na
wageni , tuwaangalie na kusimamia usalama wao licha ya kuwepo kwa
vyombo vya ulinzi na usalama,”alisema Sheikhe Kichwabuta.
Alisisitiza kwa vile waislamu wanayo dhamana kubwa ya kulinda amani na
utulivu wahakikishe sherehe hizo za kihistoria za maulidi ya Mtume
S.A.W. yanafanyika kwa amani, usalama, mshikamano na upendo miongoni
mwa waumini Kiislamu na jamii ya Watanzania.
Sheikhe Kichwabuta pia ahimiza waumini kushiriki na masheikhe
kuendelea kusema na kukutangaza jambo hilo la heri kwenye mimbari
(msikitini) na kushughulika na watu wanaoyahitaji maulidi,waachane na
wasiyoyataka ili mwisho wa siku yafanyike kulingana na hadhi ya Jiji
la Mwanza.
Aidha, Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza alhaji Hasani Kabeke alisema Kitendo
cha Mufti Abubakar Zuberi kuipa BAKWATA mkoani humu jukumu la kuandaa
Maulidi ya Mtume S.A.W. Kitaifa baada ya miaka 29 ni mtihani, ili
kuufaulu ni kuyafanikisha.
Alisema kwa sababu Watanzania waislamu na wasio waislamu
wanashirikiana kwa mambo mbalimbali ya kijamii, washirikiane kwa wenye
uwezo,wajitoe hali na mali, wenye magari ama nyumba za wageni wasaidie
kuwahifadhi wageni hao wa Mtume S.A.W. na kuwasafirisha.
Tunashirikiana na waislamu na wasio waislamu, hivyo wasio waislamu
hawajaweewa pazia (mipaka), wanayo haki ya kuchangia
Maulidi.Wajitokeze na watusaidie kuwahudumia wageni wa Mtume Muhammad
S.A.W. na si BAKWATA.Watakachotoa ni kwa ajili ya wageni hao wa
mtume,”alisema.
Kwa mujibu wa Sheikhe Kabeke jumla ya watu 10,000 wanaratajiwa
kuhudhuria kwenye sherehe hizo wakiwemo masheikhe 20 kutoka nchi za
Burundi, Kenya, Uganda na Rwanda, kuanzia Novemba 4 hadi 9, mwaka huu
huku shilingi milioni 171 zihitajika kwa shughuli hiyo.ssss
Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke (mwenye kanzu nyeupe), akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu Maalumu wa BAKWATA wa kupokea taarifa ya maandalizi ya sherehe za Maulidi ya Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza Novemba 9, mwaka huu.
Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke (katikati),akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa BAKWATA wa kupokea taarifa ya maandalizi ya sherehe za Maulidi ya Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza Novemba 9, mwaka huu.
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W. Sadiki Mshola akitoa taarifa fupi ya fedha za maandalizi kutoka vyanzo mbalimbali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Miundombinu na Mapambo, Musa Mkumbi, akitoa taarifa kwenye mkutano Mkuu Maalum wa BAKWATA mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhusu hatua iliyofikiwa pamoja na bajeti inayohitajika.
Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa BAKWATA mikoa ya Kanda ya Ziwa baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya Maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W. yanayotarajiwa kufanyika kitaifa jijini humu Novemba 4-9, mwaka huu.
Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke akifunga mkutanoMkuu Maalumu wa BAKWATA mikoa ya Kanda ya Ziwa baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya Maulidi ya Mtume Muhammad S.A.W. yanayotarajiwa kufanyika kitaifa jijini humu Novemba 4-9, mwaka huu. Picha zote na Baltazar Mashaka
No comments:
Post a Comment