Friday, October 18, 2019

PSPTB YAWAPIGA MSASA WANAFUNZI KUTOKA KENYA NA TANZANIA

BODI ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini (PSPTB) kwa kushirikiana na chuo cha Biashara (CBE) wamewakutanisha wanafunzi 60 wanaosoma kozi ya ununuzi na ugavi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, Kenya na wanafunzi kutoka nchini kwa malengo ya kubadilishana uzoefu ili kuweza kuendeleza sekta hiyo zaidi.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mkurugenzi wa fedha na mipango kutoka Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB) Paul Bilabaye amesema kuwa kusanyiko hilo la shirikisho la wanafunzi kutoka Afrika Mashariki limewakutanisha wanafunzi kutoka nchini na Chuo kikuu cha Nairobi kutoka ndaki ya biashara inayohusisha ununuzi na ugavi.

Amesema kuwa kupitia mkutano huo wamepata nafasi ya kishirikishana uzoefu baina yao na wenzao kutoka Kenya na wametumia nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini pamoja na maendeleo mbalimbali yanayoendelea kufanyika chini ya serikali ya awamu ya tano na hiyo ni pamoja na kukubaliana kuendeleza mahusiano 

Ameeeleza kuwa wameshirikiana na Chuo cha biashara cha nchini (CBE) katika kufanikisha kuwakutanisha  wanafunzi 60 kutoka nchini Kenya ili kubadilishana ujuzi katika masuala ya ununuzi na ugavi yanavyoendeshwa nchini kupiyia bodi ya PSPTB ili kuendeleza sekta hiyo zaidi.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa umoja wa wanafunzi wa masuala ya ununuzi na ugavi kutoka nchini Kenya Mercy Onyango amesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa yenye tija kwao kwa kuwa wamejifunza mengi kutoka bodi ya ununuzi na ugavi PSPTB.

Amesema kuwa ushirikiano baina ya Kenya na Tanzania uendelee ili kuweza kuendeleza sekta hiyo ya ununuzi na ugavi katika nchi hizo.

Pia Rais wa shirikisho la wanafunzi wa ununuzi na ugavi kutoka Tanzania Mrisho Ndili amesema kuwa; mkutano huo umeleta faraja kubwa hasa katika kuimarisha mahusiano baina yao na wanafunzi kutoka chuo cha Nairobi.

Amesema kuwa kuna tija ya kuanzisha umoja wa wanafunzi wa ununuzi na ugavi kuuunda shirikisho  la pamoja ambalo linatija sana kwa ukanda huo, aidha ameishukuru bodi ya ununuzi na ugavi (PSPTB) pamoja na Serikali kwa kutoa ushirikiano kwa wananfunzi wa taaalama hiyo.
 Mkurugenzi wa fedha na mipango kutoka bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akitoa mafunzo kwa wanachuo wa chuo kikuu cha Nairobi na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma kozi ya Ununuzi na Ugavi wakati wa mkutano uliolenga kubadilishana uzoefu ili kuweza kuendeleza sekta hiyo zaidi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Biashara(CBE) jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanachuo wa chuo kikuu cha Nairobi na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma kozi ya Ununuzi na Ugavi wakifuatilia mada kwenye mkutano uliolenga kubadilishana uzoefu ili kuweza kuendeleza sekta hiyo zaidi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Biashara(CBE) jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment