HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 4, 2018

Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa kufanya malipo kwa kutumia Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG)

Wateja wa Kampuni ya Tigo wa mikoa ya Kanda Ziwa sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa. 

Akiongea katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Mecky Manyama alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi na kuongeza kuwa umeleta faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza ubadhirifu na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali na taasisi za Serikali 

“Mfumo wa GePG, pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka MWAUWASA. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufurahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao.,” alisema Manyama 

“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo mkakati yetu,” alisema Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthuman Madatti 

Aliongeza “Zaidi ya wateja milioni 7 wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,” 

Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara ya Utalii, Bodi ya Utalii, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA), Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile Muhimbili, Mwananyamala na idara nyingine zaidi ya 300. 

Ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza namba ya siri ili kufanikisha muamala. 
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG)uliofanyika jijini Mwanza leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akionyesha namna ya kutumia simu ya kiganjani kufanya malipo, wakati wa uzinduzi wa  Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG), ambao utatumika kufanya malipo kwa taasisi zaidi ya 300 za Serikali kwa kutumia mtandao wa Tigo. Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti (kulia), akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ambavyo simu ya kiganjani kupitia mtandao wa Tigo inaweza kutumika kulipa malipo mbali mbali kwa taasisi zaidi ya 300 za serikali wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG)uliofanyika jijini Mwanza leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo Ally Maswanya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) , wakati wa uzinduzi wa  Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG), ambao utatumika kufanya malipo kwa taasisi zaidi ya 300 za Serikali kwa kutumia mtandao wa Tigo.Anayefuatia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo Ally Maswanya. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad