HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 13, 2018

MIRADI NANE IMEKAMILIKA NDANI YA SIKU 100 ZA DAWASA MPYA- CEO DAWASA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja  akizungumzia siku 100 za DAWASA MPYA iliyoanzia Septemba 01 2018.

Na Zainab Nyamka, lobu ya Jamii
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ameeleza kuwa ndani ya siku 100 miradi nane imekamilika kwa asilimia 100 na wananchi wameanza kuunganishiwa maji.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, ,Mhandisi Luhemeja amesema miradi yote iliyokuwa imeahidiwa kukamilika ndani ya siku 100 imeweza kufikia malengo kwa asilimia kubwa na kuunganishwa wateja wapya kutoka maeneo yaliyokuwa hayana mtandao.

Amesema, mradi wa ujenzi wa matanki ya Salasala, Bagamoyo, Changanyikeni na maeneo mengine yameshamilika na wateja wameanza kuunganishwa kwenye mfumo wa maji wa DAWASA.

"Miradi imekamilika ikiwemo ujenzi wa matanki matano ya maji yaliyopo kwenye maeneo ya Bagamoyo, Changanyikeni, Salasala na sehemu zingine, ikiwemo maunganisho ya maji kwa wateja wapya,"amesema Luhejema.

Luhemeja amesema, katika siku 100 za Dawasa, miradi nane imekamilika na takribani miradi kumi na tano (15) imeanza ikiwemo mradi wa maji Kibamba- Kisarawe utakaosaidia Dar es Salaam ya Kusini kupitia Gongo la Mboto hadi Tazara.

Amesema, mkoa wa Dar es Salaam una changamoto kubwa ya maj hususani kwenye maeneo mapya ila kwa sasa kuna mradi wa Buza umeshatandikwa bomba la inchi 16 litakaosanmbaza maji mpaka maeneo ya Yombo, Jet na Tandika.

Mbali na hilo, kuna mradi wa Kiwalani 3 ambao umeshaanza kufanyiwa kazi, mradi wa kupelekea maji Bonyokwa, Tabata Kisukuru, Saranga na kusambaza mtandao wa maji Kigamboni.

Pia, Mradi wa Chalinze upo mbioni kukamilika na kufikia Desemba 31 mwaka huu wakandarasi watakabidhi mradi huo kwa DAWASA na kazi itakayobaki ni kuanza kuweka mtandao wa maji kwa wananchi wa Mlandizi, Chalinze na Chalinze  Mboga na tayari Vizimba 97 vitaanza kutoa maji kabla ya Krismas.

Mradi wa visima vya Kimbiji na Mpera kwa sasa wataalamu wameanza kudizaini mfumo wa usambazaji kwa wananchi na mwisho wa mwezi huu DAWASA watakabidhiwa visima vitano vilivyokuwa vimekamilika tayari.

Akielezea upotevu wa maji, Luhemeja amesema kwa sasa upotevu wa maji umepungua kwa asilimia 4 kutoka 46 hadi 42 ikiwa ni ndani ya siku ya 100 na kumekuwa na ongezeko la mapato ndani ya miezi miwili.

DAWASA MPYA ilianza Septemba 01 2018 baada ya kuunganishwa kwa Mamlaka mbili za DAWASA NA DAWASCO  na kuwa na menejimenti moja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad