HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 13, 2018

Mahiga:Tuadhimishe Uhuru kwa kuwakumbuka waliopigania Uhuru huo

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga amesema kuwa wakati wa kuadhimisha Uhuru ni lazima kuwakumbuka viongozi waliopigania Uhuru huo. Mahiga aliyasema hayo wakati sherehe za Uhuru wa Nchi ya Kenya kwa Wakenya waishio Tanzania iliyofanyika katika ukumbi Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Kenya inaadhimisha miaka 55 ni kutokana na Baba wa Taifa wa nchi hiyo Jomo Kenyatta kupigana mpaka kupatikana kwa Uhuru ambao wa Kenya wanaendelea kuwa wamoja. Mahiga amesema Tanzania na Kenya zina uhusiano ambao ulitokana na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Kenya Hayati Jomo Kenyatta na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambapo mafanikio hayo ndio nchi mbili zinaendelea kufaidi. Aidha amesema miaka 55 ni mingi kwa Kenya kuendelea kulinda misingi iliyoachwa na viongozi waliopigania Uhuru.

Nae Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu amesema kuwa Tanzania na Kenya zimekuwa na historia na kufanya wananchi wa nchi mbili hizo kuwa na uchumi unaotegemeana katika biashara pamoja na Uwekezaji. Amesema kuwa Tanzania zimefungua Milango ya biashara kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Kenya kuwa na nia njema kurahisha biashara pamoja na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesema Kenya zimefungua milango kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya Uwekezaji pamoja na biashara bila vikwazo vyovyote. Katika sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Kenya viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augostine Mahiga akizungumza kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akizungumza na wageni waalikwa kutoka Balozi mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali ya Tanzania wakati wa hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa KTN, Mark Masai akitoa historia jinsi nchi ya Kenya ilivyopata uhuru wakati wa hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augostine(wa kwanza kulia) pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu wakikta keki kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augostine pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad