HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 10 December 2018

Idris Sultan avunja rekodi nyingine tenaMchekeshaji Idris sultan akiburudisha maelfu ya wakazi wa Dar es salaam na viunga vyake waliofika katika tamasha la Komedi maarufu kama SEX TOUR hivi karibuni katika ukumbi wa Club next door Arena Jijini Dar es salaam.

Mchekeshaji Deo Akiwaburdisha wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwa singe katika onesho la SEX tour Lilofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Club Next door Arena Jijini Dar es salaam.

Coy Mzungu akita burudani katika jukwaa la Sex Tour katika onesho hilo liliofanyika hivi karibuni hapa jijini Dar es salaam na kuvunja rekodi kwa maelfu ya watazamaji zaidi ya elfu 7 patika ukumbi mmoja.
Msanii wa Muziki wa Kijazi kipya Billnass akitumbuiza umati wa wakazi wa Dar es salaam waliojitokeza katika Tamasha la komedi maarufu kama SEx Tour lilofanyika hivi karibuni hapa Jijini Dar es salaam.

Jaymondy akiwavunja mbavu maelfu ya watazamaji waliojitokeza katika ukumbi wa Club next door katika Tamasha la Komedi maarufu kama Sex Tour liliofanyika hivi karibuni hapa jijni Dar es salaam.


Idris sultan akiendelea kuvunja mbavu za maelfu za wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika jukwaa la Club next door Arena katika Tamasha la komedi maarufu kama Sex Tour liliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Maelfu ya wakazi wa jiji wakifurahia burudani za wachekeshaji mbali waliotumbuiza katika onesho la Sex Tour lilofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Maelfu ya wakazi wa jiji wakifurahia burudani za wachekeshaji mbali waliotumbuiza katika onesho la Sex Tour lilofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Idris akiwa anapima afya yake katika madhimisho ya siku ya ukimwi duniani huku akiongozana na wachekeshaji wenzake kuhamasisha vijana kutokuwa na woga wa kupima na kujua hali zao.Mchekeshaji Idris Sultan amealikwa kuhudhuria tamasha kubwa la Komedi litakalofanyika mwezi huu nchini Afrika kusini lililoandaliwa na Comedy Central , moja kati ya taasisi kubwa Duniani katika tasnia ya ucheshi na uchekeshaji.

Mualiko wa Idris unakuja baada ya msanii huyo wa tasnia ya uchekeshaji kufanya Tamasha la Sex Tour ambalo liliwavuta maelfu ya wapenzi wa comedy hapa nchini .Kwa mujibu wake mualiko wa huo ni sifa kubwa kwa Taifa, baada ya bongo flava kutoboa kimataifa, sasa ni zamu ya tasnia ya uchekeshaji wa Tanzania.

Akizungumzia kuhusu tamasha la Sex Tour Idris alisema lilikuwa na lengo kuu ya kuburudisha na kuelimisha watu katika ma swala mbali mbali ya kijamii kwa kutumia Sanaa ya uchekeshaji.“Tarehe 1 December Idris Sultan aliandaa tamasha la kwanza la Sex Tour katika ukumbi wa Next Door Arena. Watu zaidi ya 7,000 walihudhuria huku wengi wakilalamika kukosa ticket.

SexTour imekua tamasha kubwa zaidi la comedy kuwahi kutokea nchini Tanzania na kufananishwa na baadhi ya matamasha makubwa ya muziki” anasema.Likibeba ujumbe "Kutokupima hakubadili matokeo"tamasha hilo lilihudhuriwa na wachekeshaji mbali mbali akiwemo Jaymondy, Mkaliwenu, Dogo pepe, Coy Mzungu, Blackpass,kitenge,Nalimi ,Optalema Deo, Max, Young Unstopable ,D comic na wengine wengi huku upande ma muziki wa kizazi kipya ukiwalishwa vyema naa Whozu na Billnass

“Changamoto za maambukizi mapya kwa vijana wa umri 15-24 bado ni kubwa, hivyo Sex Tour ilikua inalenga zaidi kushauri vijana kujali afya zao, kutokuwa na hofu ya kupima afya zao lakini pia kubadili fikra potovu za kuwa nyanyapaa wenye maambukizi,”anasema Idris

Tamash la Sex Tour lilidhaminiwa na Mfuko wa dharura wa Raisi wa Marekani wa kupambana na maambukizi ya Ukimwi (PEPFAR) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad