HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 6 December 2018

Filamu ya Uwoya, Red Light kuonyeshwa kesho Ijumaa

Baada ya uzinduzi wa Msimu wa Siku kuu na promosheni kutoka kwa Kampuni ya Star Media (T) Ltd, ambapo walitangaza rasmi nia yao ya kuisadia Bongo Movie kwa kununua filamu kadhaa na kuzionyesha kupitia chaneli yao ya Kiswahili, sasa filamu hizo zinaanza kuruka katika chaneli hiyo ya Kiswahili.
Ili kurejesha ladha ya filamu za nyumbani maarufu kama Bongo Movie, ambayo kwa muda mrefu watazamaji wameikosa. Msimu huu wa Siku kuu StarTimes wataonyesha jumla ya filamu 25 katika kipindi cha mwezi mzima wa Disemba.
Kwa wiki hii ya kwanza ya mwezi Disemba miongoni mwa filamu zitakazoonekana kupitia chaneli ya StarTimes Swahili ni Red light ambayo imemshirikisha mlimbwende Irene Uwoya ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini. 
Filamu hiyo inamuelezea kijana wa miaka 27 ambaye baba yake aliuwawa na rafiki yake huku mkewe akipona, kisa kikiwa ni pete ya utajiri. Mama na kijana wake wanaamua kuhama mji na kwenda kuishi sehemu nyingine ambako wanakutana na kijana anayewapatia habari kuhusu muuaji wa baba wa familia yao. Hivyo wanasafiri kumtafuta muuaji huyo na mwishoni wanakuta akiwa amefariki hivyo wanaichukua pete ya utajiri ambayo ilichukuliwa baada ya mauaji ya baba yao, na kuwa matajiri tena.
Filamu nyingine zitakazoonekana wikendi hii ni Agent Bavo na Akili Kichwania ambayo imemshirikisha mshekeshaji Haji Salum maarufu kama Mboto. Hii ni katika kuongeza chachu kwa wadau wengine kujitokeza na kusaidia ukuaji wa soko la filamu ndani ya nchi.
Wateja wa StarTimes wataweza kutizama filamu hiyo kwa kulipia kifurushi cha mwezi mzima cha Nyota kwa TSH 8000 tu upande wa Antenna na Tsh 11000 kwa upande wa Dish. Katika msimu huu wa Siku kuu kila watakapolipia kifurushi cha NYOTA watabustiwa hadi kifurushi cha MAMBO upande wa Antenna na SMART upande wa Dish.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad