HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 1, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA KONGAMANO LA HALI YA UCHUMI NA SIASA NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU YA UONGOZI WAKE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa Mshiriki Maalum, akizungumza na Wageni mbalimbali wakiwemo Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Viongozi wa Kiserikali, Mabalozi kutoka nchi mbalimbali, pamoja na wananchi   waliohudhuria katika Kongamano la Hali ya Uchumi na Siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano lililofanyika katika ukumbi wa Nkuruma uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Sehemu ya Watoa Mada wakiwa Wanasikiliza michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa katika Ukumbi wa Nkuruma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni Profesa Humphrey Moshi, Profesa Kitila Mkumbo, Makamu Mkuu wa Chuo Profesa William Anagisye, Profesa Rwekaza Mukandala, Profesa Martha Qorro pamoja na Profesa Hudson Nkotagu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa mshiriki Maalum katika Kongamano hilo akiandika baadhi ya Hoja katika Kongamano hilo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa Mshiriki Maalum akiwa pamoja na washiriki wengine wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Watoa Mada katika Kongamano la Hali ya Uchumi na Siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano lililofanyika katika ukumbi wa Nkuruma uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Hali ya Uchumi na Siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano wakisikiliza kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa mshiriki Maalum alipokuwa akizungumza katika ukumbi wa Nkuruma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwa nje ya Ukumbi wa Nkuruma wakifatilia Kongamano la Hali ya Uchumi na Siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa njia ya Luninga wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa mshiriki Maalum alipokuwa akizungumza katika ukumbi wa Nkuruma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa mshiriki Maalum katika Kongamano hilo akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Kisutu mara baada ya kutoka katika Ukumbi wa Nkuruma katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad