HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 10 November 2018

POLISI MKOA WA PWANI WANAWASHIKILIA WATU WANNE KWA TUHUMA ZA WIZI

Na  Mwandishi Wetu, Kibaha Pwani
WATU wanne  wanashikiliwa na  Jeshi  la Polisi Mkoa wa Pwani  kwa tuhuma za  uvunjaji wa nyumba  usiku na  kuiba katika  maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani ambapo jumla ya mali zote zilizokamatwa zina thamani kiasi cha Shilingi Mil. 18,800,000.

Watuhumiwa  hao wamekamatwa  kufuatia msako  mkali ulioendeshwa na  makachero wa kupambana  na makundi yanayojihusisha na matukio ya uvunjaji na kuiba mali za watu  katika nyakati za usiku na mchana.

Yamesemwa  hayo  na Kamanda  wa Jeshi  la Polisi Mkoa wa Pwani   ACP  Nyigesa Wankyo  amesema kuwa  majina ya watuhumiwa  yamehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi na kufanikisha kuukamata  mtandao wote wa walioshirikiana  nao katika matukio ya uvunjaji.

RPC   Wankyo alisema kuwa katika msako huo wamefanikiwa  kukamata vitu  mbalimbali  amabvyo ni luninga  kumi   za aina  mbalimbali ( zote Flat Screen) , jenereta kubwa mbili zenye thamani ya sh.6, 500,000, jenereta hizo ni aina ya  Euro Power  EP.6500E na Boss  BG-2500.

Vitu vingine vilivyokamatwa  katika msako huo ni  pamoja na  deki mbili,ving'amuzi viwili, spika mbili  music system mbili, home theatre, rimoti sita, speaker twiter mbili, flash moja, kapeti za chini ya sakafu mbili, stendi moja ya vyombo na extention moja.

Aidha Kamanda amesema  kuwa wamemkamata mtuhumiwa mmoja akiwa na lita 200 za mafuta ya dizeli  ambapo alikutwa na madumu kumi yenye ujazo wa lita 20  mafuta hayo alikua ameiba katika karakana ya mradi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) iliyopo eneo la Soga  Wilaya ya Kipolisi Mlandizi.

Pia amewaasa  wale wote  wanaohujumu  mradi wa  mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa kuiba mafuta  kuacha mara moja tabia hiyo kwani Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani  hawatakuwa na muhali  nao na mtu  yeyote atakayejaribu kujihusisha  na vitendo  vya wizi  tutawakamata  na kuwafikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

"Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kijiji cha  Mperamumbi akiwa amepakia  mafuta  hayo  kwenye pikipiki aina ya SANLG namba MC.197BJD.Mtuhumiwa anashikiliwa  kwa mahojiano zaidi  kwa lengo la  kubaini walem wote ambao  amekuwa  akishirikiana nao katika wizi huo  wa  mafuta  na atafikishwa  Mahakamani kujibu tuhuma hizo mbili zinazomkabili" alisema Wankyo.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani  limekamata bhangi kiroba kimoja  kilichokua kinasafirishwa kwenda kuuzwa, katika tukio hulo mmiliki wa  pikipiki  yenye namba za usajiliMC951  BSA anaombwa  kujisalimisha  kwenye kituo  chochote cha Polisi ndani ya siku  tatu vinginevyo atasakwa  popote  pale aliko ili kujibu  tuhuma za kusafirisha  bangi ambayo aliitelekeza ikiwa  kwenye  pikipiki  hiyo  baada ya  kugundua  anafuatiliwa na  askari  wa jeshi la polisi.

"Kutokana na  matukio haya Jeshi  la Polisi  Mkoa wa Pwani  tunatoa wito  kwa wananchi  kuwa  wabia  katika  suala zima  la  ulinzi  shirikishi kwenye maeneo  tao ili  kuweza  kukabiliana  na matukio ya uvunjaji wa sheria..Pia tunatoa  rai kwa  wananchi  wa Mkoa wa Pwani kuwafichua  wale wote wanaoshirikiana  na wahalifu  kwenye maeneo  yao kwani  haiwezekani  mahali pakavunjwa  katika mtaa bila  ya kuwepi na wenyeji  wanaowafahamu alisema  RPC Wankyo.

"Natoa wito kwa  wananchi kuacha tabia ya  kununua  vitu vya mikononi bila kupewa risiti  ya kile  wanachokinunua, wale wote ambao  watakutwa  na mali  ya wizi  nao tutawachukulia hatua  kali za  kisheria  ili iwe mfano kwa wengine"alisema Kamanda huyo.
 Kamanda  wa Jeshi  la Polisi Mkoa wa Pwani   ACP  Nyigesa Wankyo akiwa na baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi  akizungumza na waandishi wa habari

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad