HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 7 November 2018

KAILIMA AKUTANA NA WASEMAJI NA WAKUU WA TEHAMA WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

Naibu  Katibu  Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ramadhani Kailima amekutana na  Wasemaji na Wakuu wa vitengo vya Tehama wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kikao kilichofanyika Dar es Salaam, na kuwataka watendaji hao kuboresha mifumo ya utoaji  taarifa na elimu kwa umma ya Idara zao.  
Katika kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani, Kailima amewataka watendaji hao kukaa na kutengeneza mfumo wa pamoja utakaoziunganisha Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi ya katika kutoa taarifa na elimu kwa umma hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi  wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020. 
Amewataka Wasemaji na Wakuu wa hao wa vitengo vya Tehama kuhakikisha kuwa wanaihabarisha jamii kuhusiana na matukio na shughuli zinazofanywa na Idara zao ili jamii ipate ufahamu wa kutosha kuhusiana na majukumu ya idara hizo.
Wasemaji na Wakuu wa vitengo vya Tehama waliohudhuria kikao hicho ni wa kutoka Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji. 
 Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima akiongea  na Wasemaji na Wakuu wa vitengo vya Tehama wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Naibu katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi katika kikao kilichofanyika Dar es Salaam

Wasemaji na Wakuu wa vitengo vya Tehama wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Naibu katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi (hayupo Pichani) (Picha na Jeshi la Polisi)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad