HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 7 November 2018

ALI KIBA AKUBALI KUSHIRIKI WASAFI FESTIVAL, MOFAYA KUDHAMINI TAMASHA HILO


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


Msanii wa muziki wa Bongofleva Ali Kiba amemjibu msanii mwenzake Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz'  kuptia ukurasa wake wa Instagram kuwa amekubali mualiko wa kwenda kushiriki katika tamasha la Wasafi Festival.


Katika ujumbe wake Ali Kiba amesema kuwa, ameshukuru kwa kupata mualiko wao ila hataweza kushiriki kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kuzindua kinywaji chake cha Mofaya Energy.

Mbali na hilo Kiba amemuomba Diamond kudhamini tamasha hilo ili kusongesha gurudumu la muziki wa Tanzania.


"Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrink ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa . Management #RockstarAfrica yangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa "


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad