HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 24 October 2018

WATALAAM WA MAJI ENDESHENI VIKAO KAZI KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIRADI-AWESO

 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), watatu kutoka kushoto, akikata utepe tayari kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa  Katesh utakaohudumia zaidi ya wakazi 40,000 na kutarajiwa kuhudumia wakazi wa Katesh  kwa zaidi ya miaka 20.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Katesh. Anayeshuhuda ni mkuu wa wilaya ya Hanang’ Mhe. Joseph Mkirikiti 
 Naibu Waziri wa Maji akisikiliza maelezo ya mradi wa maji wa Endasaboghechan ulifanikishwa kwa ushirikiano na Kampuni ya Bia ya Serengeti. Mradi huo unatumia nishati ya jua.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb)  akiongea na wakazi wanaotarajia kunufaika na mradi wa maji wa Endagaw-Gedangu ambapo Mhe Aweso amewahakikishia wananchi kuwa Mkandarasi wa mradi atalipwa kiasi cha shilingi milioni 184 akamilishe mradi na huduma ya maji ipatikane mara moja.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akisaidia kuchota maji katika eneo la Waranga. Hata hivyo, Mradi wa maji wa Waranga unatarajia kukamilika siku za usoni hivyo kuondoa adha ya wananchi kuchota maji katika mashimo.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akikagua chujio la mradi wa maji Katesh.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akipanda ngazi kukagua tanki la mradi wa maji Gehandu. Waziri amesisitiza lazima watalaam kwanza wajiridhishe na vyanzo vya maji kabla ya kujenga miundombinu ya maji.


Watalaam wa maji nchini wametakiwa kuendesha vikao kazi mara kwa mara ili kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama kwa wakati, pia wahandisi wa maji wa mikoa kuhakikisha wanapitia miradi ya maji kabla ya utekelezaji wake. 

 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema hayo wilayani Hanang’ wakati akikagua miradi ya maji na kusisitiza watalaam wa maji kukutana katika vikao ni fursa ya kubadilisha uzoefu katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maji, pia kujifunza zaidi ili kuleta ufanisi katika kazi.
Mhe. Aweso amesema haiwezekani mtaalam wa maji anakaa ofisini na kupokea ripoti za mradi bila kujiridhisha kwa kutembelea mradi, na kuwashirikisha watalaam wenzake anapoona baadhi ya maeneo kazi haiendi kama inavyotakiwa.  

Mhe. Aweso katika ziara hiyo ameweka jiwe la msingi la mradi wa maji Katesh ambao ukikamilika utakua na uwezo wa kuhudumia zaidi ya wakazi 40,000, na utakua na uwezo wa kutoa huduma kwa zaidi ya miaka 20. 

Mhe. Aweso wakati wa hafla hiyo amewaelekeza watalaam wote wa mabonde ya maji nchini kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa kwa kuwashirikisha wananchi ili kuhakikisha rasilimalimaji inatumika kwa matumizi endelevu kwa maendeleo ya wananchi wote.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na; mradi wa maji Lambo, mradi wa maji Endasaboghechan, mradi wa maji Endagaw, mradi wa maji Waranga na mradi wa maji Gehandu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad