HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 18 October 2018

Wakulima wachangamkia fursa za Sim Akaunti ya Benki ya CRDB

 Meneja usambazaji wa Sim Akaunti wa benki ya CRDB, Yusuph Mwenda akizungumza jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa kuchezesha droo ya promosheni ya SimAkaunti, iliyofanyika leo, Mikocheni jijini Dar es salaam.

MKAZI wa mkoani Ruvuma, Zenidius Luwo na mfanyabiashara wa nafaka kutoka Arusha, Hanset Munisi leo wameibuka washindi kwenye promosheni ya SimAkaunti inayondeshwa na benki ya CRDB.

CRDB imekuwa ikitoa zawadi kwa wateja wake wanaojisajili na kutumia huduma hiyo ambapo huwapatia fedha tasrimu. Luwo aliibuka mshindi wa shilingi milioni mbili huku Munisi akipata milioni moja. Tangu kuanzishwa kwa promosheni hiyo mwezi huu, wakulima wameoongoza kujishindia zawadi kutoka benki hiyo.
Akizungumza baada ya kuchezesha droo ya kuwapata washindi hao, Meneja Masoko wa benki hiyo, Ariel Mkony, alisema mbali na washindi hao wawili, pia benki hiyo imewapata washindi wengine 10 wa shilingi 100,000.

"Lengo letu ni kuona wateja wetu wananufaika na bidhaa zetu.. SimAkaunti inaweza kuwasaidia sana watu wa aina mbalimbali, kuanzia mtu mmoja mmmoja na hata vikundi," alisema Ariel.

Aidha, mmoja wa washindi hao, Munisi, alisema fedha hizo alizozipata kama zawadi zote ataziingiza kwenye biashara yake ya vyakula.

Kwa upande wake, Meneja usambazaji wa Sim Akaunti wa benki hiyo, Yusuph mwenda, alisema wataendelea kuiboresha huduma hiyo kuwanufaisha zaidi wateja wao. Promosheni hiyo itadumu kwa kipindi cha miezi minne ambapo wataendela kutoa zawadi kwa wateja wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad