HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 22 October 2018

VITILIGO SI UGONJWA, WALA MADHARA YA VIPODOZI NA HAINA TIBA

 Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii


KUNA muonekano ambao jamii umekuwa ukiunasibishwa na matumizi yaliyopitiliza ya vipodozi, ugonjwa au kasoro ila ni hali ya kawaida inayoweza kumpata mtu yeyote. 

Vitiligo ni hali ya ngozi kupoteza rangi yake na kuacha madoa/ mabaka katika sehemu fulani za mwili hasa zile zinazopata mwanga wa jua haraka kama mikono, uso na macho.

Hali hii husababishwa na seli zinazoipa ngozi rangi ya mwili zijulikanazo kama Melanocyte kufa au kushindwa kufanya kazi.

Daktari John Bergman kutoka Marekani ameeleza kuhusu hali hiyo na kusema kuwa seli zinazoipa ngozi rangi ya mwili zikifa mtu hukumbwa na Vitiligo na sababu za tatizo hilo hazijafahamika licha ya baadhi ya wataalamu kueleza kuwa Vitiligo husababishwa na mwili wenyewe kwa baadhi ya seli kuvamia kazi katika sehemu nyingine ya mwili, wengine husema kuwa seli hizo za Melanocyte zinazotengeneza rangi ya mwili hujiharibu zenyewe na baadhi ya wataalamu hueleza kuwa Vitiligo husababishwa na mwili kuchomwa sana na jua licha ya kutothibitisha.

Dalili za vitiligo ni pamoja na kuanza kutokea kwa mabaka katika sehemu mbalimbali hasa macho, mikono, miguu na uso.

Pia Vitiligo huweza kugundulika kwa kutokea kwa rangi nyeupe au kijivu kwenye nyusi, kope au ndevu na hata kupotea kwa rangi ya retina (eyeball) na rangi kwenye tishu ndani mdomo na pua.

Inashauriwa kuwa  mwanga wa jua ni muhimu hasa asubuhi na jioni  kwa dakika 20 na matibabu ya Vitiligo ni kurudisha rangi ya ngozi inayopotea  ila sio kuzuia kuendelea kupungua kwa rangi ya ngozi.

Ukweli kuhusu Vitiligo; Rangi ya nywele huweza kutabiri nguvu ya Melanin, huathiri watu wa kila aina ila huonekana sana kwa watu wenye rangi nyeusi na huwapata watu katika umri wowote kabla ya kufikia umri wa miaka 20 bila kujali jinsia wala kabila na ni ngumu kutabiri kuenea kwake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad