HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 22 October 2018

Upelelezi dhidi ya kesi ya aliyekuwa mke wa bilionea msuya wakamilika

BAADA ya kusota rumande kwa zaidi ya miaka miwili, hatimae upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella umeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, upelelezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika. 

Wakili wa Serikali Mwandamizi,  Patrick Mwita ameieleza hayo leo Oktoba 22,2018 Mahakama wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa. 

Akitoa taarifa hizo, Wakili Mwita  amedai kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika hivyo, wanaiomba Mahakama ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washtakia maelezo ya mashahidi na Vielelezo (Committal).

"Mheshimiwa Jalada la kesi hii limeshatoka kwa DPP na sasa tunalo hapa,  hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya mashahidi na Novena amedai Mwita.

Kufuatia taarifa hiyo, wakili wa utetezi Peter Kibatala ameomba Mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe fupi ili wateja wake waweze kusomewa maelezo hayo. 

Baada ya kusikiliza maelezo hayo Hakimu Simba amahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi mwaka huu. 

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kumuua kwa makusudi Dada  wa marehemu bilionea, Erasto Msuya, Aneth Msuya.

Kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo, Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada,  wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad