HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 18 October 2018

TFDA YAIKUTANISHA TBS , GCLA, TAFFA KUJADILI UBORESHAJI WA UINGIZAJI WA BIDHAA NCHINI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii 
MAMLAKA ya chakula na dawa nchini (TFDA) kwa kushirikiana na shirika la Viwango nchini (TBS) , Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) chama cha mawakala wa forodha nchini (TAFFA) wamekutana na kujadili namna ya kuimarisha na suala zima uingizaji wa bidhaa nchini. 

Akizungumza katika mkutano huo kaimu mkurugenzi mkuu wa TFDA Agnes Kijo ameeleza lengo la mkutano huo ni kukumbushana ili kuweza kusaidia kuboresha huduma kwenye taasisi hizo katika utoaji wa mizigo kwa kufuata sheria kwani bila kufanya hivyo hawatafikia malengo ya taifa. 

Amesema kuwa waingizaji wa mizigo na mawakala wa forodha lazima wawe pamoja katika kulinda afya za wananchi. 

Ameeleza kuwa wamekaa na wadau wengi wakimemo wenye viwanda na awamu hii wameamua kukaa na mawakala hao wa uingizaji mizigo nchini ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuweza kuzitatua na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao. 

Agnes ameeleza kuwa wote wapo kwa ajili ya kuijenga nchi hivyo ni lazima kuhakikisha kila mamlaka inasimamia ipasavyo majukumu yao ili kuhakikisha kuwa suala la uingizaji wa mizigo kwa kuzingatia umuhimu wa wadau hao na amehaidi kuwa taratibu zitaenda kufanyika kielektronoki ili kurahisisha mchakato mzima. 

MKemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ,Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelince Mafumiko amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa wadau hao hasa katika uingizaji wa kemikali kwa ajili ya viwanda na ameeleza kuwa wadau hao ndio huwezesha uingizwaji wa bidhaa hizo hivyo ni fursa kwao katika kutoa taratibu na mrejesho wa changamoto katika kutekeleza ufanisi, na changamoto zitakazotolewa na wadau watazifanyia kazi na amesema kuwa huo ni mwanzo mzuri katika utoaji wa huduma. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa shirika la viwango (TBS) Lazaro Msasalaga amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuongeza ufanisi katika mchakato wa utoaji wa mizigo bandarini pamoja na changamoto zinazogusa taasisi zao na kuendeleza uchumi wa nchi. 
Kaimu Mkuruergnzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo akizungumza na wadau wa wakala forodha katika mkutano wa kujadili masuala mbalimbali ya utaoaji wa huduma katika bandari kwa bidhaa za vyakula uliofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na vyombo vya habari wakati wa mkutano wa uliowahusisha wakala wa uingizaji wabidhaa ndani ya nchi kupitia kwa mawakala wa forodha juu ya uingizaji wa bidhaa hizo na mamlaka za utoaji wa vibali uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto Daud Msasi akizungumza katika utaoaji wa salam kwa katibu mkuu huyo mawakala wa forodha uliofanyika jijinI Dar es Salaam.

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TFDA Emmanuel Alphonce akitoa maada katika mkutano wa mawakala wa forodha namna ya utoaji wa vibali pamoja na ukaguzi katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya washiriki katika mkutano wa wadau wa forodha katika mkutano wa ulioitishwa na TFDA kwa ajili ya uboreshaji wa huduma katika uondoshaji wa mizigo katika bandari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad