HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 5, 2018

Tanzania mwenyeji Michuano ya AFCON 2019

Na Shamimu Nyaki -WHUSM

Serikali imesema Jiji la Dar es Salaam ndio litakalotumika katika mashindano ya AFCON mwakani kutokana na kuwa na miundombinu inakayokidhi mahitaji ya michuano hiyo.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo amesema baada ya wakaguzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afika (CAF) kuridhia kuwa jiji hilo lina miundombinu rafiki  ikiwemo viwanja, hoteli pamoja na huduma za afya.
“Maandalizi ya AFCON2019 yanaendelea vizuri tayari wakaguzi kutoka CAF wameshafanya ukaguzi wa awali na wamechagua Dar es Salaam ndio itakayotumika katika michuano hiyo ambapo mechi ya ufunguzi na ile ya fainali zitafanyika katika Uwanja wa Taifa”. Alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha ameongeza kuwa viwanja vingine vitakavyomika ni uwanja wa Uhuru ambao upo katika ukarabati wa kuwekewa nyasi bandia na kurekebisha miundombinu mingine pamoja na uwanja wa Chamazi ambao nao utafanyiwa ukarabati kulingana na matakwa ya CAF, na uwanja utakaotumika katika mazoezi mojawapo ni uwanja wa Jakaya Kikwete  Park.
Pia Dkt Mwakyembe alieeleza kuwa maandalizi ya Kampeni ya Uzalendo na Utaifa yanaendelea ambapo mwaka huu kauli mbiu ni “Kiswahili Uhai wetu,Utashi Wetu” na  kilele kitakua Disemba 08 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Vilevile Waziri Mwakyembe amewataka wamiliki wa visismbuzi nchini kufuata sheria ya urushaji wa matangazo   kulingana na leseni zao ikiwa ni pamoja na kuelewa kuwa leseni ya kuandaa vipindi ni tofauti na ile ya kurusha matangazo.
Ameendelea kueleza kuwa usikivu wa TBC umeendelea kuimarika ambapo mpaka sasa Wilaya 102 zinapata matangazo ya shirika hilo kwa uhakika na Serikali inaendelea na juhudi za kufikisha matangazo kwa wananchi wengi zaidi.
“TBC imeimarisha usikivu na inaendelea kufanya hivyo ambapo kwa sasa Wilaya za mpakani zinapata matangazo hayo na awamu inayofuata ni mikoa ya Songwe,Simiyu,Mtwara,Tanga Wilaya ya Lushoto na  visiwani Zanzibar ambapo pia  tayari fedha zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa studio ya kisasa Jijini Dodoma.” Ameongeza Dkt. Mwakyembe.
Hata hivyo amewataka wanahabari nchini kufuata misingi ya Sheria ya Habari inayowataka kufuata weledi na maadili ya taaluma hiyo na kutambua kuwa Sheria hiyo inawataka kuwa na elimu ya kuanzia Stashahada.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad