HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 26 October 2018

RC MAKONDA AMUAGIZA AMBER RUTTY KUFIKA KITUO CHA POLISI LEO KABLA YA SAA 12 JIONI

Na Agness Francis, blogu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemuagiza mwanadada Amber Rutty anayejihusisha na masuala ya muziki wa bongo fleva nchini kufika katika kituo chochote cha Polisi hapa jijini leo  kabla ya saa 12 Jioni.

Rc Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha ya mwanadada huyo na kuandika haya :

"Wakati TCRA wakijipanga kuchukua hatua, mimi namtaka mwenye picha hii kufika kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu na eneo lake kabla ya saa 12 jioni. Na ukifika waambie umeitwa na RC Makonda watakupatia ujumbe wako" ameandika  Makonda.

Hii inakuja baada kwa kosa la matumizi mabaya ya mtandao  linalomkabili kwa kusambaza Video ya  yenye maudhui ya kingono
na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuleta sintofahamu kubwa kwa Wanajaamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad