HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 30, 2018

POLISI, TRA KILIMANJARO WANASA KIWANDA FEKI CHA KUTENGENEZA POMBE KALI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamisi Issah (anayeongea na Simu ) akiongozana na Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kilimanjaro ,Godfrey Kitundu walifika kwenye nyumba inayoaminika kuwa kiwanda cha kutengeneza Pombe kali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Hamisi Issah akitizama baadhi ya chupa ambazo zimendaliwa kwa ajili ya kujaza kimiminika cha Pombe kali.
Sehemu ya Mitambo iliyopo ndani ya kiwanda hicho kilichopo katika wilaya ya Himo ambacho kinaaminika kuhusika katika kutengeneza Pombe kali bila ya kufuata taratibu.
Anayedaiwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho akitoa maelezo kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Hamisi Issah pamoja na Meneja Msaidizi wa TRA Kilimanjaro anayeshughulikia masuala ya forodha ,Godfrey Kitundu ndani ya kiwanda hicho.
Sehemu ya Mitambo iliyopo ndani ya kiwanda hicho.
Baadhi ya Chupa zilizokutwa ndani ya kiwanda hicho zikiwa hazina stika ya TRA.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamisi Issah akijadili jambo na Meneja Msaidizi wa TRA -Kilimanjaro ,Godfrey Kitundu mara baada ya kukagua kiwanda hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamefanikiwa kukamata kiwanda  cha kutengeneza Pombe kali ambacho kimekuwa kikizalisha bidhaa hiyo bila ya usajili.
Moja ya dira za serikali ya awamu ya tano ni kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda ,hata hivyo baadhi ya wafanyabiahara watafsiri Dira hii tofauti kwa kuamua kuanzisha Viwanda bila ya kufuata matakwa ya Sheria na taratibu za nchi.

Hali hii imejidhihirisha mkoani Kilimanjaro katika mji mdogo wa Himo baada ya Polisi,TRA na TFDA kubaini uwepo wa kiwanda bandia kinachozalisha Pombe kali .
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamisi Issah amesema jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na idara nyingine za serikali kuhakikisha kodi ya serikali inapatikana pamoja na kuhakiki ubora wa bidhaa kwa ajili ya afya ya watumiaji.
Zoezi la kubaini uwepo wa viwanda bandia katka mkoa wa Kilimanjaro ambapo katika siku za karibuni viwanda vilivyogundulika ni vile vinavyotengeneza Pombe za kienyeji na Pombe kali ,baadhi  vikiwa katika wilaya ya Rombo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad