HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 26, 2018

MIKAKATI YA DAWASA KATIKA KUWAPATIA HUDUMA YA MAJI MKOA WA PWANI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Tenki maji Bagamoyo ni moja ya mifumo ya matenki matano yaliyojengwa chini ya mradi wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji. Mradi huu unaotekelezwa kwa ushirikiano na Serikali ya India kwa thamani ya jumla ya dola za Marekani milioni 39.



Mkandarasi anayejenga huu mradi ni Jain Invngetic ya India akishirikiana na subcontracts Shanxi ya nchini China na mshauri ni WAPCOS kutoka India. Mradi pia umehusisha ujenzi wa vituo vinne vya kusukuma pampu za maji, ujenzi wa matanki, ufungaji wa pampu na transfoma katika vituo hivyo pamoja na ulazaji wa mabomba ili kupeleka maji katika matenki hayo.

Aidha mradi pia umehusisha ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji katika maeneo ya Salasala, Wazo, Bunju na ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji kati ya maeneo yaMbezi na Kiluvya na kwa upande wa Bagamoyo bomba maalum la kupeleka maji katika eneo la viwanda EPZA pamoja na bandari mpya limelazwa. Chini ya mradi huu, jumla ya mabomba ya kipenyo cha kati ya milimita 63 na 400 kwa urefu wa jumla ya kilometa423.899 yamelazwa, mwisho wa mkataba huu ni tarehe 31/10/2018.


 Tunaamini kwa kufanya hivi wametoa mchango stahiki katika kuwezesha eneo letu la huduma hususani Bagamoyo kutekeleza wajibu wake wa kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati.



Tenki la Bagamoyo pamoja na matenki mengine matatu yaliyopo Mabwepande, Wazo na Salasala yana uwezo wa kuhifadhi lita milioni sita za maji kila moja na tenki la Changanyikeni lina uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni tano. Matenki yote yaliyopo Dar es salaam yamegawanywa katika sehemu mbili zenye ujazo sawa ili kuwezesha usafi, matengenezo ama ukarabati kufanyika katika sehemu moja na kuruhusu sehemu ya pili kuendelea kutumika na hivyo kutokuathiri huduma kwa wananchi.

Tenki hili la Bagamoyo, tofauti na matenki mengine chini ya mradi huu, limegawanywa katika sehemu nne na halina kituo cha kusukuma maji. Hii ni kwa sababu maji yake yanatoka hapa jirani katika toleo la bomba kuu kutoka Ruvu Chini ambao ndiyo mtambo wa maji mkubwa kuliko yote nchini wenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 270 kwa siku.

Pampu zake zina uwezo wa kusukuma lita 3,125 kwa sekunde na kurusha maji mita 75 kwenda juu. Hivyo basi maji yanaweza kufika katika tenki hili liliopo jirani bila tatizo. Bagamoyo ni mji ambao upo katika uwanda wa tambarare hivyo tenki hili lipo katika eneo lililo na muinuko mkubwa kuliko maeneo mengine mjini hapa Bagamoyo; hivyo litawezesha maji kufika katika maeneo yote yanayolengwa kwa msukumo (pressure) wa viwango vinavyotakiwa.

DAWASA imekuwa ikishirikisha wadau mbalimbali katika kutekeleza miradi yake, ikiwa ni pamoja na viongozi wa wananchi. Katika moja ya ziara za ukaguzi wa ujenzi wa mradi huu, Mheshimiwa Mbunge wa Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa aliomba tenki dogo la zamani lililopo katika ofisi za Mkuu wa Wilaya liunganishwe na Mfumo huu ili liweze kuhudumia wananchi waliopo jirani na tenki hili; na kuruhusu tenki hili kuhudumia wakazi waliopo mbali ikiwemo na maeneo ya kibiashara na mahoteli ya kitalii kwa ajili ya maendeleo ya mji wa Bagamoyo na Taifa kwa ujumla. DAWASA ni Mamlaka sikivu na yenye kupenda kuwatumikia Wananchi, hivyo napenda kutoa taarifa rasmi kuwa Mkandarasi alielekezwa kufanya kazi hii, hivyo atakamilisha kati ya 31/10/2018, baada ya kusafisha tenki (disinfection) wakati tukisubiri Mkandarasi wa kujenga distribution/mtandao apatikane chini ya mradi wa World Bank.

Tenki hili la Bagamoyo linatarajiwa kuhudumia wakazi wa mji wote wa Bagamoyo navitongoji vyote vinavyozunguka mji pamoja na vitongoji vya Bongwa, Nianjema, Magomeni, Mangesani, Mianzini, Tandika, Mahotelini, Majani mapana, Majengo, Kidongo chekundu, Kisingani, Saigoni, Mantep, Mji Mpya, Kisutu, Kimala Ng’ombe, Block Pukuni, Sanzale, Polisi, Magambani, Kaole, Chumvi, Makarani, Hospitali, Chunguuni, Msalabani na maeneo ya Shule ya sekondari na chuo kikuu kishiriki_Marian.

Mradi wa Maji wa EPZ tayari bomba la kipenyo cha 400mm limelazwa umbali wa Km 5
la kipenyo cha 400mm limelazwa kwa ajili ya maeneo ya viwanda, Mkandarasi ilitakiwa kukabishi kabla ya tarehe 31/10/2018.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuonyesha Makamu ww Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu tenki la maji la mradi wa maji wa Bagamoyo unaotekelezwa na Mamlaka hiyo chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati alipotembelea ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milion sita kwa siku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad