HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 25, 2018

JET YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI JUU YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI

Na Said Mwishehe,  Globu ya Jamii
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini(JET)kimeamua kuwajengea uelewa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu uhifadhi wa mazingira na wanyamapori nchini

Akizungumzia semina hiyo inayofanyika wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Mkurugenzi Mtendaji John Chikomo amefafanua lengo kubwa la mafunzo ni kuwajengea uelewa waandishi hao kuhusu sekta yenyewe na kuhamasisha uhifadhi wa wanyamapori.

Pia amesema lengo lingine la semina hiyo ni kutangaza utalii wa ndani ili uweze kueleweka kimataifa na kuwashawishi sekta binafsi kuwekeza kwenye uhifadhi na utalii.

Chikomo amefafanua ni matarajio yao baada ya mafunzo hayo waandishi watakuwa na uelewa mpana kuhusu uhifadhi wa mazingira na wanayama pori na baada ya semina hiyo waandishi watapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo kwa kutembelea hifafhi za wanyamapori.

"Tumeanza na mafunzo haya na baadae tutaendelea na hatua nyingine zinazofuata ikiwemo ya waandishi husika kwenda kufanya uchunguzi kwa kuandika habari zinazohusu mazingira na uhifadhi.

" Mafunzo haya ni sehemu ya mradi unaoshughulikia kuendeleza uhifadhi mazingira ambapo ndani yake pamoja na kuangalia mafanikio pia unashughulika na changamoto zinazohusu uhifadhi,"amesema.

Wakati huo huo baadhi ya watoa mada wameeleza kwa kina kuhusu historia ya uhifadhi wa wanyamapori na mazingira pamoja na sheria mbalimbali zilizopo kwa nyakati tofauti na namna ambavyo zinafanyakazi nchini.

Mmoja wa watoa mada Stanslaus Nyambea kutoka Timu ya Wanasheria wabobezi kwenye masuala ya mazingira( LEAT) amezungumzia sheria ya fidia kwa watu wanaopata madhara kutoka kwa wanyama aidha iwe kwa kusababisha kifo au kuharibu mali ambapo sheria hiyo inaonekana kuwa na mlolongo mrefu wa kupata fidia.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mjadala kwenye semina ya waandishi wa habari za mazingira nchini inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani .Semina hiyo imeandaliwa na JET.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini(JET) John Chikomo akifafanua jambo kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sekta ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina ya mafunzo ya waandishi wa habari za mazingira.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) wa kwanza kushoto pamoja na waandishi wengine wa vyombo vya habari wakisikiliza mada kwenye semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi kuhusu sekta ya uhifadhi wa wanyamapori.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) na watoa mada.
Mwakilishi kutoka USAID Protect Symphrose Makungu akizungumza kwenye semina ya Waandishi  wa habari za mazingira ambayo imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) nchini ya ufadhili wa USAID Protect
Mwanasheria kutoka Timu ya Wanasheria  waliobobea katika  mazingira (LEAT) Stanslaus Nyembea akitoa mada kwenye semina ya waandishi wa habari za mazingira inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad