HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 26 October 2018

Dkt. Ndumbaro amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa China

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya watu wa China Mhe. Wang Ke, katika mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kwenye sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, biashara, kilimo na teknolojia. Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndumbaro amemshukuru Mhe. Wang Ke, kwa kuendelea kuliwakilisha Taifa lake vyema hapa nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dar es Salaam Tarehe 25 Octoba, 2018.
Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Ndumbaro na Mhe. Wang Ke 
Sehemu ya maafisa wa Ubalozi wa China wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Ndumbaro na Mhe. Wang Ke. 
Balozi Wang Ke akimwelezea Dkt. Ndumbaro zawadi ya sahani yenye mchoro wa maua 
Dkt. Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wang Ke (wa tatu kutoka kushoto), kulia ni maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kushoto ni Maafisa Ubalozi wa China. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad