HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 6 February 2018

AZAM FC, SIMBA SC VITANI KESHO UWANJA WA TAIFA

Na Agness Francis,  Globu ya jamii 
MABINGWA Afrika Mashariki na kati Azam FC watakuwa wageni dhidi ya vinara aa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba Sc katika mchezo wao wa 2 mzunguko wa 2.

Mchezo huo  utakaorindima kesho  katika  dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao Mzizima jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema wapo vizuri katika kumkabili mnyama Simba na kuhakikisha wanaondoka  na ushindi wa maboa ili kuweza  kuwasogelea  vinara hao wenye pointi 38.

Wakati  Azam FC wakiwa nyuma kwa pointi 33 wakiwazidi Yanga SC  wenye alama 31.

"Tunajua ni mchezo  utakaokuwa mgumu dhidi ya Simba SC kwa kuwa wana kikosi kipana na kizuri ila sisi tumejipanga kuhakikisha tunarudi na  ushindi nyumbani na vijana wapo vizuri wote wana morari ya  kufanya vizuri  katika mchezo huo "amesema Jaffary Maganga. 

Aidha amesema katika mchezo huo wa vuta ni kuvute dhidi ya wekundu hao  wa Msimbazi wataendelea kuwakosa wachezaji wao ambao wapo majerui, Waziri Junior na Joseph Kimwaga  ambaye bado hayupo vizuri mpaka sasa kwa kuwa  alifanyiwa upasuwaji wa goti hapo siku za nyuma.. 

"Mchezaji wetu Aboubakar Salum  maarufu kama (Sure boy) atarejea mchezoni Kesho akiwa amemalizia kutumikia adhabu yake ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa 16 wa kukamilisha mzunguko wa 1 uliochezwa pale Chamazi na Mabingwa watetezi YangaSC na kusababisha  kukosa mechi iliyopita dhidi ya NdandaFC," amesema Maganga.
Msemaji Mkuu AzamFc, Jaffary Iddy Maganga akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi zao Mzizima Jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi yanayoendelea katika kikosi chake ambapo kesho watavaana  na mnyama simba katika Dimba la Uwanja wa Taifa majira ya saa 10 jioni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad