HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 23, 2017

WANANCHI WA KATA YA GAIRO WAOMBWA KUENDELEA KUCHANGIA SEKTA YA ELIMU

 Na Mwandishi Wetu. 
Wananchi wa Wilaya ya Gairo wameombwa kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika maendeleo ya sekta ya elimu ili kupata matokeo bora.

Kauli hiyo imetolea Disemba 21, 2017 wakati wa kuwasomea mapato na matumizi ya michango ya elimu kwa wananchi wa Kata ya Chakwale na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati akabidhi tani mbili na nusu ya mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno.

Mhe. Mchembe alisema kuwa saruji hiyo itasaidia kuendeleza zoezi la kufyatua matofali ambapo mpaka sasa wameshafyatua matofali 5,600.

Aidha amekaribisha wadau mbalimbali kuendelea kuchangia baada ya wananchi kuchangia shilingi milioni 33 ndani ya miezi mitatu.

"Hamasa ni kubwa kwani watoto wanatembea kilometa zaidi ya Sita kwenda shule. Hili limekuwa ni jaribu kwa watoto wa kike. Vijana wa bodaboda wanatuharibia watoto wa kike. Shule ikiwa karibu itapunguza changamoto hii.

Mkuu wa Wilaya aliipongeza Kamati ya Ujenzi kwa kazi nzuri ya kukusanya michango ya maendeleo na kazi ya ujenzi ambayo tayari imeanza. Tunategemea kuanza ujenzi mapema Januari katika eneo la ekari 15.

Wilaya ya Gairo ina madarasa zaidi ya 30 yote yamejengwa kwa nguvu ya wananchi hadi ngazi ya boma, bado kuezeka. Madarasa haya ni nje ya madarasa 16 yaliyomalizika ndani ya mwaka mmoja.

"Mpaka sasa hatuna darasa la nyasi wala wanafunzi wanaokaa chini. Tumemaliza nyumba za waalimu 8, maabara 6 na tuna maboma yanahitaji nguvu ya ziada," alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akimkabidhi mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili iweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu na nyumba za walimu. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo.
Wananchi wa Kata ya Chakwale wakisomewa taarifa ya michango yao shilingi milioni 33. Aidha Wenyeviti wa vijiji vitatu walirudishiwa shilingi milioni 10 ikiwa ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo ya vijijini.
Mkuu wa Wilaya akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Mhe.  Maneno ili awagawie Wenyeviti. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili ili awagawie Wenyeviti wa kata yake. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad