HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 25, 2017

WAFUGAJI BUKOMBE MKOANI GEITA WAWALALAMIKIA ASKARI WANYAMA PORI LA AKIBA KIGOSI

Wafugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, wamewalalamikia askari wa pori la Akiba la Kigosi Myobosi kwa madai ya  kuwanyanyasa pindi wanapokamata ng'ombe zao katika pori hilo.

Wakiongea mwishon mwa wiki ,mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Hamisi Ulega,wafugaji hao wamesema kuwa Mifugo yao inauzwa bila kufuata utaratibu pindi inapokamatwa kwenye pori hilo na matokeo yake wafugaji wanabaki Maskini.

"Magufuli anafanya kazi nzuri sana na hatuamini kabisa kuwa hapendi Mifugo,lakini kuna baadhi ya watendaji wake sio waadilifu kabisa,askari wa Pori la akiba Kigosi Myobosi wakikamata ng'ombe hawatupi fursa ya kulipa faini,badala yake wanataifisha Mifugo yetu na kuipiga mnada bila kufuata utaratibu wa serikali uliowekwa na sisi tunabaki Maskini"alisema mfugaji mmoja.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Mkoa wa Geita Bw.Hamisi Mashaka Biteko ameiomba serikali kutafuta masoko ya uhakika ya mifugo Ili  wafugaji wewe na uhakika wa soko la Mifugo yao.

"Tunaomba serikali ijenge viwanda vya kutosha vya kuchakata nyama Ili wafugaji wenye Mifugo mingi waweze kuuza Mifugo yao,inayobaki wafuge kwa tija"

Kwa Upande wake naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Ulega amesema kuwa Sheria ya Maliasili na utalii inaruhusu kupigwa mnada Mifugo yote inayoingia kwenye mapori ya akiba. lakini wamepeleka mswada Bungeni ili kuzipitia upya sheria hizo .

"Katika Bunge la mwezi wa pili 2018,sheria hizo zitapitiwa upya,nawaombeni sana ikifika wakati huo mjipange vizuri nanyi mtoe maoni yenu"

Awali katibu tawala wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Bw.Paul Cheyo, akitoa taarifa fupi ya Wilaya hiyo alimwambia Mhe.Ulega kuwa wao wametekeleza zoezi la kitaifa la upigaji chapa mifugo kwa Asilimia 73.

"Halmashauri inaendelea na zoezi la upigaji chapa mifugo.Wilaya yetu ina jumla ya ng'ombe 130,750, hadi sasa ng'ombe waliopigwa chapa ni 95,743 sawa na asilimia 73".alisema Cheyo.
 Naibu Waziri wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla  Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali baada ya kupokea  taarifa fupi ya  Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
 Naibu Waziri wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla  Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali na wafungaji  Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
 .Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji  Mkoa wa Geita Bw.Hamisi Mashaka Biteko  (kushoto)akizungumza katika mkutano huu.
 Mmoja wa wa wafungaji wa akitoa kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Wizara  ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla  Ulega, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
 Sehemu ya viongonzi mbalimbali na wafungaji waliofika katika mkutano huo.

 Sehemu ya viongonzi mbalimbali na wafungaji waliofika katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad