HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 4 December 2017

WADAU WAKUTANA KUJADILI SUMU KUVU KATIKA ZAO LA MAHINDI

Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
Umoja wa Afrika kupitia Program ya Udhibiti wa Aflotoksini  Barani Afrika (PACA) imeandaa kongamano la udhibiti  wa sumu kuvu katika bara la Afrika juu ya kuzuia ongezeko la Aflatoksini katika vyakakula (Mahindi)

Akizungumza katika Mkutano huo wa Wadau uliofanyika nchini, Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, Raymond Wigenge amesema kuwa kuwepo Aflatoksini  katika vyakula unasababisha madhara  katika usalama wa chakula, uhakika wa chakula na ukuaji wa biashara ya vyakula Afrika hivyo kuathiri afya za watu na maendeleo yao.

Amesema inakadiriwa watu milioni 208 katika bara la Afrika wanategemea Mahindi kama chakula kikuu ambapo sumu kuvu inapatikana katika zao la mahindi .

Amesema katika ya nchi 22 duniani ambazo zimekuwa na sumu kuvu katika mahindi nchi 16 zipo barani Afrika na zao la chakula zinategemea mahindi.

Aidha amesema inakadiriwa kuwa katika mwaka 2014 nchi za  ilipata hasara ya dola za kimarekani milioni 670 kwa kushindwa kuuza vyakula katika jumuiya ya ulaya kutokana na kudhibiti Aflatoksini.

Wigenge amesema inakadiriwa kuwa asilimia 30 ya wagonjwa saratani ya Ini wanapata kupitia ulaji vyakula vyenye Aflatoksini.

Amesema TFDA imekuwa ikifanya katika utoaji wa elimu juu ya sumu hiyo pamoja na kuendelea kubuni teknolojia juu ya kudhibiti sumu hiyo katika kuwalinda walaji wa kuwa na usalama  wa chakula.
 Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Raymond Wigene akizungumza na waandishi habari juu ya sumu kuvu katika mahindi katika mkutano wa Umoja wa Afrika kupitia Program ya Udhibiti wa Aflotoksini  Barani Afrika (PACA) jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wadau wa Umoja wa Afrika kupitia Program ya Udhibiti wa Aflotoksini  Barani Afrika (PACA) katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja Umoja wa Afrika kupitia Program ya Udhibiti wa Aflotoksini  Barani Afrika (PACA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad