HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 28, 2017

TOCHI ZA TRAFIKI ZIMESAIDIA KUDHIBITI MWENDO KASI BARABARANI, KUPUNGUZA AJALI: SACP MUSILIMU

Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii
JESHI la  Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litaendelea kutumia tochi kwa ajili ya kudhibiti mwendokasi huku likihimiza watuamiaji wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani nchini. 

Limetumia nafasi nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo wamefanikiwa kusimamia sheria, hivyo ajali zimepungua ikilinganisha na miaka iliyopita.

Hayo yamesemwa leo, jijini Dar  es  Salaam na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu wakati akitoa takwimu za kupungua kwa ajali  hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka. 

Kamanda Musilimu amesema usimamizi mzuri wa  sheria za usalama baraarani umesaidia kupunguza ajali na kuongeza wataendelea na jukumu lao ili kukomesha ajali. 

Amesema ajali nyingi ambazo zinatokea si  mpango wa  Mungu bali ni uzembe wa madereva na watumiaji wengine wa barabara hizo. 

"Naomba niwaambie wapo wanaosema ajali zinazotokea barabarani na kusababisha vifo na majeruhi ni mpango wa Mungu, si kweli ila zinatokana na uzembe wa madereva. 

"Kwa sasa tunahimiza watumiaji wa barabara kufuata sheria za usalama barabarani.Wapo wanaolalamikia uwepo wa tochi, naomba wafahamu hatutaacha kuzitumia kwani zimetusaidia sana kupunguza ajali,"amesema Kamanda Musilimu. 

Ameongeza uwepo wa tochi umesaidia kuwafanya madereva kutokwenda mwendo kasi ingawa bado wapo wengine wanaenda kasi na wamekuwa wakikamatwa na kuchukuliwa hatua. 

Amesemaa kwa usimamizi mzuri wa sheria na madereva kuwa na uelewa mpana wa matumizi mazuri barabarani, imesaidia kukomesha ajali.

 Kamanda Musilimu amefafanua kwa muda mrefu kumekuwa na utamaduni wa kutokea ajali nyingi kipindi cha mwisho wa mwaka na mwanzoni mwa mwaka lakini wamefanikiwa kudhibiti ajali hizo. 

"Mwishoni mwa mwaka na mwanzoni mwa mwaka havina tofauti na vipindi vingine, hivyo wananchi wasiwe na hofu yoyote, "amesema Kamanda Musilimu. 

Ametaja chanzo cha ajali ni mwendo kasi, ulevi na uzembe, lakini kwa kusimamia sheria wamefanikiwa kupunguza makosa ya barabarani. 

Alipoulizwa uwepo wa trafiki wengi wenye tochi kiasi cha kuonekana kero, jijini Dar  es Salaam Kamanda Musilimu amesema wameamua kuweka tochi hizo baada ya kuona ajali za watu kugongwa zimekuwa nyingi. 

Ametoa mfano wa eneo la Kawe Darajani kulikuwa na matukio ya watu kugongwa lakini baada ya kuweka tochi hakuna matukio ya ajali tena.Pia ameongeza maeneo yote yenye tochi ajali zimepungua. 

Kuhusu kufungiwa leseni 88 kwa madereva waliobainika kufanya makosa barabarani,katika mwezi huu,amesema sheria inamruhusu kufungia leseni kwa kipindi cha miezi sita.

"Madereva ambao tumefungia leseni zao hawataruhusiwa kuendesha mabasi ya abiria wala magari makubwa ila wanaruhusiwa kuendesha magari madogo. 
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani,  Fortunatus Musilimu akizungumza katika makao makuu ya kikosi hicho jijini Dar  es Salaam leo, kuhusu kupungua kwa ajali kipindi hiki cha mwisho wa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad