HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 20, 2017

RPC AIPONGEZA SGA KWA WELEDI, KUJALI WAFANYAKAZI

Kampuni ya SGA Security imeadhimisha miaka 33 tangu ianze shughuli zake nchini Tanzania huku ikiwatunuku wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa muda mrefu na kupongezwa na Jeshi la Polisi kwa hatua hii. Shughuli ya kuwatambua wafanyakazi hawa ilihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, SACP Jumanne Muliro katika ofisi za SGA Masaki ikiwa ni moja ya majukumu yake kuhakikisha makampuni binafsi ya ulinzi na usalama yanaendeshwa kwa viwango vinavyotakiwa.
 Kampuni hiyi iliunda kikundi maalumu kijulikanacho kama ‘Club 20’ ambacho kinajumuisha wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 20. Kwa sasa kampuni ya SGA Security imeajiri wafanyakazi zaidi ya 5,100 Tanzania na kuifanya iwe moja ya makampuni makubwa ya usalama nchini. SACP Muliro aliipongeza SGA kwa kujali masilahi ya wafanyakazi na kuongoza kwa mfano huku akisisitiza kuwa makampuni mengi ya ulinzi na usalama hayafuati utaratibu uliowekwa ikiwemo mafunzo, usimamizi na mishahara huku akitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa SGA. 
 Mgeni rasmi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni SACP Jumanne Muliro akizungumza jambo kabla ya kukabidhi tuzo kwa wafanyakazi wa kampuni ya SGA katika kuadhimisha miaka 33 tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya ofisi za SGA.

“Ni jambo la kupongezwa sana kwa kuwa kampuni yenye wafanyakazi zaidi ya 50 walioitumikia kampuni kwa zaidi ya miaka 20,” alisema. Alisema SGA ndio ilikuwa kampuni ya kwanza ya binafsi ya ulinzi na usalama kuanziswa Tanzania na imedhihirisha kuwa kuwajali wafanyakazi ndio chanzo cha mafanikio. 
“Nimefahaishwa kuwa wafanyakazi walioitumikia SGA kwa zaidi ya miaka kumi ni zaidi ya 1,500 jambo ambalo linastahili pongezi,” alisema huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na makampuni binafsi ya ulinzi na usalama kuhakikisha mkoa unakuwa salama na kuongeza kuwa walinzi wanafanya kazi kubwa katika kuzuia ujambazi. 
Naye Mtendaji Mkuu wa SGA Group, Jules Delahaije aliupongeza uongozi wa SGA nchini kwa kuhakikisha wafanyakazi wanaitumikia kampuni kwa muda mrefu na pia kwa kuwatambua na kuwatunuku waliofanya kazi muda mrefu. Aliwapa wafanyakazi hao ngao maalumu za kuonesha utumishi wao kwa zaidi ya mika 20. 
“Tukiwa na wafanyakazi zaidi ya 18,000 duniani kubwa kwetu ni watu. Tumewekeza sana katika mafunzo na pia tumehakikisha tunawalipa wafanyakazi wetu vizuri kabisa ikilinganishwa na makampuni mengine ili tuwajengee mazingira bora ya kazi na pia tuwe nao kwa muda mrefu,” alisema.
   
Mkurugenzi Mkuu wa SGA Group, Bw. Jules Delahaije akizungumza jambo wakati wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa kuadhimisha miaka 33 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo ambapo RPC wa Kinondoni, Jummane Muliro alikuwa mgeni rasmi.

Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania Eric Sambu alisema katika miaka 33 ambayo kampuni hiyo imefanya kazi Tanzania, imeshuhudia ukuaji mkubwa hasa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa sababu ya mikakati waliojiwekea na kujituma kwa wafanyakazi ili waweze kukidhi matarajio ya wateja. Alisema kubwa kabisa katika mafanikio yao ni utendaji wa wafanyakazi ambao ni waaminifu na waadilifu katika utendaji wao.
“Mazingira ya sokola ndani yametupa darasa la kutosha na imetufanya tuwawezeshe wafanyakazi wetu ipasavyo ili waweze kukidhi matarjio ya wateja kama mazingira ya sasa yanavyotulazimisha kufanya ambayo kwetu sasa ni jambo la kawaida kabisa,” alisema. “Tunaendelea kuboresha huduma zetu na kuwekeza zaidi katika teknolojia na tumeweza kutambuliwa katika ubora yaani ‘ISO certification on Quality Management System’ kuanzia 2001 na hivi karibuni pia tumepokea cheti cha Afya na Usalama yaani since ‘Occupational Health and Safety ISO 18001 Standard.’
 Alisema kampuni hiyo hadi sasa ina magari zaidi ya 224 na matawi 12 ambayo yana ofisi zenye vifaa vya kisasa na wataalamu wenye uwezo mkubwa wa kutumia vifaa hivyo kote nchini, “ alisema Sambu. 
 
Meneja Rasilimali Watu wa SGA Tanzania Ebenezer Kaale akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa wafanyakazi wake wakati kampuni hiyo ikiadhimisha miaka 33 tangu kuanzishwa kwake iliyofanyika kwenye ofisi za makao makuu ya SGA jijini Dar es Salaam.

Meneja Rasilimali Watu wa SGA Tanzania Ebenezer Kaale, ambaye aliandaa shughuli hiyo, alisema wafanyakazi wengi wa kampuni hiyo wanahusika na usafirishaji wa fedha, kazi ambayo inahitaji uadilifu mkubwa na weledi.
“Kwa kweli wafanyakazi wetu wanastahili pongezi kubwa katika hili kwani tunasafirisha fedha kwa asilimia takriban 90 ikilinganishwa na makampuni mengine ya ulinzi na usalama,” alisema. SGA inatoa huduma mbalimbali ikiwemo ulinzi kwa kutumia walinzi, vifaa vya umeme, huduma za dharura, ufuatiliaji, usafirishaji wa vifurishi na fedha.
 Baadhi ya wafanyakazi walioitumikia SGA Security kwa zaidi ya miaka 20 wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea tuzo zao huku kampuni hiyo ikiwa inaadhimisha miaka 33 tangu kuanzishwa kwake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad