HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 8, 2017

Naibu Waziri Nditiye atoa siku 14 kwa Tipper kuunganisha bomba kwa TPA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditye, ametoa siku 14 kuhakikisha bomba la mafuta la Kimataifa linalosambaza mafuta (TIPPER), liwe limeunganishwa kwenye mfumo unaodhibitiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili serikali iweze kupata mapato sahihi.

Kutokana na bomba la tipper kuunganishwa katika bandari kumesababisha serikali kupata mapato kwa kampuni hiyo kujisimamia yenyewe.

Akizungumza katika ziara ya kikazi aliyoifanya bandarini hapo jana,  Nditye amesema, TPA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na EWURA wafanye uchunguzi wa haraka kufahamu upotevu wa mapato ya serikali yaliyotokana na Tipper kujiunganishia mafuta kutoka kwenye meli bila kupitia katika kituo cha Kurasini Oil Jet (KOJ).

Amesema Tipper  wamekiuka maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaaliwa yaliyolewa Februari mwaka jana  ya kutaka waunganishe bomba lao katika mfumo wa TPA ili kufahamu kiwango cha mafuta wanayoyachukua.

" Wizi wa waziwazi  tangu Februari mwaka jana alipoagiza Waziri  Mkuu  hadi leo TIPPER mmeshindwa kuunganisha bomba lenu hali inayochangia mapato ya Serikali kuzidi kupotea," alisema Nditye.

Amesema TIPPER waliagizwa na waziri ndani ya mwezi.mmoja wawe wamejiunga katika.mfumo huo lakini cha ajabu maaagizo yamekiukwa hali inayoashiria bado kuna ujanja unaendelea.

Amesema haiwezekani TIPPER wakajiunganisha wenyewe halafu wakajisimamia wao.kufahamu kiwango cha mafuta ya dizeli na ya kula wanayotumia.

Aliagiza pia TPA iimarishe ulinzi kwa mtoa taarifa za upotevu wa mafuta hayo na endapo atapata madhara Serikali.itachukua hatua.

Awali Meneja Mafuta wa Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni Paul Paul alisema TIPPER wamekiuka.agizo la waziri Majaliwa ambapo hadi sasa hawajajiunganisha katika mfumo wa bomba linalodhibitiwa na TPA.

Amesema hadi sasa makampuni yaliyounganishwa katika mfumo wa TPA ili kuangalia kiasi cha mafuta kinachotumika ni pamoja na Lake Oil,  Moil, Hass pamoja na World Oli/Sahara/Kobil.

Paul alisema kitendo cha mita za mafuta ya TIPPER kudhibitiwa na wenyewe linatakiwa liangaliwe kwani lina athari.

 Mkurugenzi Msaidizi wa TIPPER, Paul Mzava alisema, walipokea.maelekezo kutoka kwa Msajili wa hazina kusitisha kuhamishwa kwa bomba hilo mara baada ya waziri Majaaliwa kutoa agizo. Alisema taarifa hizo walizipeleka kwa uongozi wa TPA kwa maandishi.

Mzava alisema kuhamishwa kwa bomba linalomilikiwa na TIPPER kulipeleka kwenye mfumo wa TPA kuna umbali wa mita 400 hivyo waliona ni gharama kulihamisha. Alisema pia waliona katika kituo kile cha KOJ kitahamishwa muda wowote hali itakayochangia hasara.

Akijibu hoja hizo, Mhandisi Deusdetit Kakoko alisema alichokuwa anafahamu ni kuwa tayari TIPPER wamejiunga na mfumo wao.

 "Binafsi nilipewa taarifa kuwa tayari TIPPER wamejiunga katika mfumo wetu kinyume na hapo sina taarifa nyingine,"alisema Kakoko.

Alisema kutokana na hali hiyo atahakikisha anafuatilia undani jambo hilo pamoja na.kuwawajibisha watendaji waliokwenda.kinyume na agizo hilo.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Ashasta Nditye akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) katika ziara yake alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini  (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko  akitoa taarifa za utendaji wa mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Atashasta Nditiye (Kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mamlaka ya Bandari jijini Dar es Salaam.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Atashasta Nditiye akizungumza katika ujenzi wa scanner ya ukaguzi katika bandari ya Dar es Salaam.
Naibu  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano ,Mhandisi  Atashasta Nditiye akifanya majumuisho baada ya kufanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad