HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 20 December 2017

Mlimani City Mall yatangaza zawadi ya X-Mas na Mwaka Mpya

Katika kusherehekea Sikukuu za X-Mas na Mwaka Mpya, uongozi wa Mlimani City kwa kushirikiana na wafanyabiashara wenye maduka ndani yake umetangaza ofa maalumu kwa wateja  wake watakaofanya manunuzi katika msimu huu wa sikukuu.
Ofa hiyo inatoa fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali ambazo zimegawanywa kwa makundi matano ambapo kila wiki washindi 20 watajishindia vocha yenye thamani ya kufanya shoping kwa vitu vya thamani ya Shilingi 100,000 lakini pia watakuwa mwameingia moja kwa moja kwenye droo kubwa ya mwisho ambayo mshindi wa kwanza atajishindia vocha ya manunuzi ya bidhaa za nyumbani yenye thamani ya Shilingi Milioni 10, na mshindi 5 watajinyakulia vocha yenye thamani ya shilingi milioni 1, kila mmoja.  
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja mkuu wa Mlimani City Ndugu Pastory Mrosso alisema kuwa washindi wa kila wiki watafanya manunuzi katika duka lolote ndani ya Mlimani City kwa kutumia vocha zao.
Promosheni hii maalumu imeanza Desemba 15 na inatarajia kufikia mwisho Januari 14, 2018, ambapo droo kubwa ya kupata mshindi wa kwanza wa Vocha yenye thamani ya Shilingi milioni 10.
Meneja huyo aliwaomba watanzania kuendelea kufanya manunuzi yao katika maduka ya Mlimani City, kutokana na kuwajali wateja wake na kutoa huduma zinazokwenda na wakati na hasa katika kipindi hiki cha X-Mas na Mwaka Mpya.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Secta Binafsi nchini Tanzania(TPSF), Godfrey Simbeye akichagua kuponi ya mshindi wa kwanza wa promosheni ya ‘Fanya shoping mlimani City na ushinde zawadi katika kipindi hiki cha siku kuu ya Chrismass na Mwaka Mpya iliyozinduliwa rasmi jana Mlimani City.Kushoto kwake ni Meneja wa Mlimani City, Pastory Mroso na wengine mabalozi wa kampeni hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Secta Binafsi nchini Tanzania(TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya ‘Fanya shoping mlimani City na ushinde zawadi katika kipindi hiki cha siku kuu ya Chrismass na Mwaka Mpya iliyozinduliwa rasmi jana Mlimani City.Kulia ni Meneja wa Mlimani City, Pastory Mroso.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad